Rais Yoweri Museveni ameongoza Uganda kwa ziadi ya miaka 30
Mahakama ya Kikatiba inasikiliza kesi iliyoletwa na upande wa upinzani kufuta marekebisho ya katiba ambayo yanatoa ukomo wa miaka ya kuwa rais.
Wabunge waliipigia kura wa kishindo mwaka uliopita kufuta ukomo wa miaka 75.
Ilimaanisha kuwa Rais Yoweri Museveni mwenye miaka 73, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, anaweza kuwania tena mwaka 2021.
Mawakili wa upinzani walitoa hoja kuwa marekebisho hayo yaliingizwa "kinyemela" hadi kuwa sheria, na bunge halikufuata kanuni zilizopaswa katika kuweka marekebisho hayo.
Ulinzi umeimarishwa katika eneo la mahakama liliopo katika jiji la Mbale, mashariki mwa Uganda, na baadhi ya barabara zimefungwa kuepusha machafuko.
Hii ni mara ya kwanza ombi la haki la kikatiba linasikilizwa , anaripoti mwandishi wa BBC Patience Atuhaire kutoka jiji kuu la Kampala.
Miongoni mwa waomba haki ni wabunge wa upande wa upinzani,chama cha wanasheria Uganda na asasi za kiraia.
Wabunge wapigana makonde Uganda
Wanasema marekebisho hayo hayana msingi kwa sababu yalipitishwa wakati vurugu ilitokea kwenye vipindi ambapo walinzi waliovaa nguo za kawaida waliwatoa wabunge bungeni.
Pia wanatoa hoja kuwa Bw Museveni anataka kuwa rais wa maisha na kuwa mabadiliko hayo yanakiuka misingi ya kidemokrasia, utwala unamlikiwa na watu.
Washirka wa Museveni wanasema marekebisho hayo yanatoa ubaguzi wa kiumri na yalipitishwa baada ya kupata ushauri wa Umma.
Chama tawala cha National Resistance Movement kiliongoza mabadiliko hayo kupitia bunge na Bw Museveni akatia saini na kuifanya sheria.
Bw Museveni alishinda awamu ya tano mwaka 2016 katika uchaguzi uliodaiwa kuwa na dosari.
Ukomo wa awamu mbili ulifutwa mwaka 2005 ili kumwezesha awanie ofisi tena
Maoni