Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KOCHA MBELGIJI: NIPENI TAIFA STARS NIIPELEKE KOMBE LA DUNIA 2022

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuanza mchakato wa kumsaka kocha mpya wa Taifa Stars, Mbelgiji, Adel Amrouche ameibuka na kufunguka kuwa, akipewa nafasi ya kuinoa timu hiyo, ataipambania ishiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Mbali na Kombe la Dunia, pia Mbelgiji huyo mwenye asili ya Algeria, amesema ataanza kwanza kupambana kuhakikisha Taifa Stars inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Cameroon.
Hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, alisema mchakato huo wa kumsaka kocha, unaendelea vizuri ambapo wanaanza kupitia wasifu ‘CV’ mbalimbali za makocha walioomba nafasi hiyo baada ya kocha wa sasa, Salum Mayanga kumaliza mkataba wake tangu mwezi uliopita.
Akizungumza na Championi Jumatatu , Kocha Amrouche aliyezaliwa Machi 7, 1968 katika Mji wa Kouba, Algiers nchini Algeria, amesema: “Nina uzoefu na soka la Afrika, nimefundisha timu ya taifa ya Kenya na Burundi, lakini pia kwenye klabu, nimefundisha DC Motema Pembe ya DR Congo na USM Alger ya Algeria.
“Najiamini na ndiyo maana nimekuwa nikitamani sana kuifundisha Taifa Stars ambayo imekuwa na kiu kubwa ya mafanikio, kama nikifanikiwa kuwa kocha wa timu hiyo, nitahakikisha mwakani tuna­shiriki Afcon, kisha 2022 lazima twende kushiriki Kombe la Dunia. Hayo yote yanawezekana kwani ikiwekwa mikakati madhubuti nadhani hakuna kitakachoshindikana.”


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...