WAJUMBE NANE WA KAMATI KUU CHADEMA WATUMBULIWA


Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini leo Mei 13, 2025 imetengua uteuzi wa wajumbe 8 wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walioteuliwa baada ya kikao cha Baraza Kuu la Taifa cha tarehe 22 Januari 2025 siku moja tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hiko.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani cha Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa amefanyia kazi malalamiko ya Lembrus K. Mchome kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 4(5)(a)na(b) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na Kanuni ya 31(2)(3) ya Kanuni za Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa za Mwaka 2019 (Political Parties (Registration and Monitoring) Regulations, 2019 GN. 953) amebaini kuwa malalamiko ya Mchome ni ya ukweli kwamba kikao cha Baraza Kuu la Taifa la CHADEMA kilichofanyika tarehe 22 Januari 2025 kilikuwa batili, kwa sababu kilikuwa hakina akidi inayotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006 toleo la 2019. Vilevile, hata kama kikao hicho.
Ameomgeza kuwa hata kama kikao kingekuwa halali, uthibitishaji wa viongozi uliofanywa na kikao hicho ulikuwa batili, kwa sababu watu ambao siyo wajumbe wa kikao hicho walikuwa ndani ya ukumbi na baadhi walipiga kura hivyo CHADEMA wametakiwa waitishe kikao kingine cha Baraza Kuu la Taifa kujaza nafasi za viongozi zilizokuwa wazi kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba na Kanuni za CHADEMA, kisha wawasilishe taarifa kwa msajili kwa mujibu wa Sheria
Viongozi waliotenguliwa ni pamoja na -:
John Mnyika – Katibu Mkuu,
Amani Golugwa -Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Ally Ibrahim Juma – Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar).
Wengine ni Godbless Lema, Rose Mayemba,
Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh,
Dk. Rugemeleza Nshala (Mwanasheria Mkuu wa chama) ambao ni Wajumbe wa Kamati Kuu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU