Tume za Haki za Binadamu kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Burundi zakutana

MTEULE THE BEST


Tume za Haki za Binadamu kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Burundi zimekutana nchini Tanzania kujadili namna ambavyo tume hizo zinaweza kusimamia viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Utawala bora, amani na haki za binadamu.

Akifungua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utatoa tadhmni ya miaka 3 ya utendaji wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, sambamba na kutoa mapendekezo mapya kwa nchi hizo hasa katika kutatua migogoro na kulinda amani.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Marry Massay amesema tume hizo zinawajibu wa kuhakikisha haki inazingatiwa, kutatua migogoro baina ya wananchi na viongozi wao na kushugulikia malalamiko.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu kutoka nchini Burundi Jean Baribonekeza amesema hali ya Burundi kwa sasa imeimarika tofauti na mwaka mmoja ulipita ikiwa ni juhudi ya tume hiyo katika kushugulikia mgogoro wa kisiasa uliopo nchini humo ambapo amewakumbusha wanasiasa kulinda usalama wa raia wanapotekeleza majukumu yao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU