Rais Samia amefungua Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC)

May be an image of 2 people, dais and text 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo June 09,2023 amefungua na kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC), Ikulu Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA kwenye Sekta za Umma ili ianze kusomana ambapo ameahidi kuwa sio zaidi ya miezi sita RAISkinachotokea Bandarini atakuwa anaweza kukisoma akiwa Ikulu.
May be an image of 1 person and dais

Rais za Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Juni, 2023.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA, mifumo yetu haisomani, taarifa hazioani, kazi tunayokwenda kufanya kwa nguvu kubwa sasa ni kufanya mifumo ndani ya Sekta ya Umma isomane pia iwe na vigezo vya Kimataifa”

“Changamoto zilizotajwa hapa hizo za Kariakoo na nini ni kwamba mifumo yetu haijaweza kuchukua taarifa zote hizo, kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha mifumo yetu inabeba taarifa zote hizo ili tuweze kuwa na taarifa nyingi ambazo zitapelekwa kufanya maamuzi, hiyo ni kazi mbele yetu kwa upande wa Serikali na ninawaahidi nadhani sio zaidi ya miezi sita tutakuwa tunasoma kinachotokea Bandarini nakisoma Mimi Ikulu huku”

“Mafanikio makubwa tumeyapata kupitia Royal Tour lakini Kuna changamoto kwamba Wageni wanaokuja mwakani na mwaka unaofuata watakosa mahali pa kulala kama tusipochangamka kujenga Mahotel sasa hivi kwahiyo Sekta binafsi hiyo ni fursa muhimu “

“Niombe upande wa Serikali tupunguze michakato kwenye kutoa vibali vya ujenzi wa Mahoteli sijui mara NEMC hajatoa ruhusa sijui nani kazuia nini!?, tuharakisheni kwasababu Watu watakaokuja mwakani na mwaka utakaofuata hawana pa kulala”

“Kubwa zaidi kwenye Sekta yenyewe kufanya marekebisho, takwimu zinaonesha Wageni waliokuja mwaka jana ni 30% tu wamerudi mwaka huu hii, means Watu wanakuja wanasema Tanzanja hatuji tena pamoja na vivutio tulivyonavyo, tukaliangalie hilo ili wakija warudi na washawishi wengine kuja”

“Kwa upande wa booking za Wageni takwimu zinaonesha Wageni wengi sana, hofu yetu mahali pa kulala”


mteulethebest

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU