MTEULE THE BEST
Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa maeneo maalum mjini Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa.
Kiongozi huyo wa dini aliwasili katika kituo hicho cha polisi siku ya Ijumaa akiwa na wakili wake Abdallah Safari.
Bwana Mambosasa siku ya Alhamisi alimwagiza Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi aliyotoa.
Kulingana na kamanda huyo , Kiongozi huyo wa dini alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo akamatwa
Maoni