Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ICG yataka kusogezwa mbele uchaguzi nchini Kenya

MTEULE THE BEST

Shirika la kimataifa linaloshughulikia mizozo - International Crisis Group, ICG limemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, Wafula Chebukati kutolea ufafanuzi kauli aliyotoa kwenye mkutano wa waandishi wa habari Oktoba 18 kwamba ni vigumu kwa uchaguzi mpya wa urais utakaofanyika Oktoba 26 kuwa huru na wa haki, kutokana na mazingira yalivyo kwa sasa. Limemtaka mwenyekiti huyo kuiomba mahakama ya juu kuongeza siku kati ya 30 hadi 45, ili kuruhusu kupangwa kwa tarehe mpya ya uchaguzi bila ya kukiukwa kwa katiba.
Shirika hilo limeangazia maamuzi ya mahakama kuu ya Januari mwaka 2012 iliposogeza mbele uchaguzi kwa miezi sita, hatua ambayo ilisaidia kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na haki.
Shirika hilo limesema, mahakama ya juu inatakiwa kulipatia upendeleo suala hili la kuongezwa kwa siku za kuandaa uchaguzi, baada ya mwenyekiti wa tume ya IEBC, kukiri mwenyewe kwamba tume yake haiwezi kuthibitisha iwapo kutafanyika uchaguzi wa haki ndani ya muda uliopangwa.
Kutokana na kwamba ni taasisi za bunge ama mahakama ya juu zenye uwezo wa kuruhusu kuahirishwa, na kwa kuzingatia kwamba bunge litahitaji sio chini ya wiki mbili kupitisha muswada wa kuongeza siku 60 ili kufanyika uchaguzi mpya, mwito huo katika wakati kama huu unaweza tu kutolewa na mahakama
Mahakama itatakiwa kueleza wazi kwamba Uhuru Kenyatta atasalia mamlakani hadi uchaguzi mpya utakapofanyika
.
Shirika hilo limesema iwapo mahakama itakubali kusogeza mbele uchaguzi, itatakiwa kueleza wazi kwamba Rais Uhuru Kenyatta atasalia madarakani hadi pale uchaguzi mpya utakapofanyika. Katiba haielezi kuhusu nani atashika madaraka wakati ambapo uchaguzi unafanyika baada ya siku 60, baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa awali.
Kulingana na ICG, kufanyika upya kwa uchaguzi wa urais unaotarajiwa Oktoba 26 kumeibua kitisho kipya cha mzozo wa kisiasa nchini Kenya. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametangaza hatashiriki, mmoja wa makamishna wa tume ya IEBC Dr. Roselyn Akombe hivi karibuni amejiuzulu na kuondoka nchini humo, huku mwenyekiti wa IEBC akiashiria kwamba hawezi kuhakikisha kutafanyika uchaguzi wa haki ndani ya muda uliopangwa.
Wasiwasi wa kutokea kwa machafuko mabaya kati ya wafuasi wa vyama viwili vikuu, ama kati ya vikosi vya usalama dhidi ya makundi yanayotaka kuzuia uchaguzi pia unazidi kuongezeka. Kuendelea kwa mchakato wa kuandaa uchaguzi huku kukiwa na wasiwasi kama huu kunaweza kuongeza mgawanyiko na kuendeleza uadui ambao tayari uligharimu maisha ya wengi na uchumi wa nchi hiyo.
Kenya ilikuwa ikiangaliwa kwa jicho ala matumaini miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki panapohusika na suala zima la Demokrasia . Lakini matukio ya baada ya uchaguzi wa rais Agosti 8 yamesababisha maswali kadhaa na hasa baada ya mahakama ya juu kubatilisha matokeo ya uchaguzi hu yaliompa ushindi rais Uhuru Kenyatta. Mahakama ilisema katika uamuzi wake Septemba mosi kwamba uchaguzi huo ulikuwa na dosari kubwa na kuamuru urudiwe. Kutokana na utata uliopo tangu wakati huo, linalosub iriwa ni ikiwa uchaguzi huo mpya utafanyika kama ilivyopangwa na tume Oktoba 26.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...