Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mahakama ya Juu kusikiliza kesi muhimu

MTEULE THE BEST
 Uchaguzi Kenya 2017: Mahakama ya Juu kusikiliza kesi muhimu
Mahakama ya juu nchini Kenya leo Jumatano itasikiliza kesi ya dharura iliyowasilishwa na wapiga kura watatu dakika za mwisho wakidai kuwa Kenya haiko tayari kufanya uchaguzi huo.
Mahakama imeombwa kuingilia kati na kuamua - iwapo uchaguzi wa marudio utafanyika..
Wanataka uchaguzi huo uahirishwe.
Rais Uhuru Kenyatta anasema uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa siku ya Alhamisi.
Muungano wa upinzani chini ya kinara Raila Odinga umetaka wafuasi wake wasusie zoezi hilo, ukiutaja kuwa uchaguzi usioweza kuwa wa huru na wa haki.
Odinga amesema Serikali ya Kenya na tume ya Uchaguzi zimeshindwa kushughulikia mapungufu yaliyosababisha mahakama ya juu zaidi nchini humo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Agosti.
Uchaguzi Kenya: Tume yasema wagombea wote watashiriki
Kenyatta akutana na mkuu wa uchaguzi Kenya
Kwa nini Roselyn Akombe alijiuzulu IEBC
Hatua hiyo inajiri baada ya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurejelewa.
Kuna utata kati ya sheria za uchaguzi, katiba na vile mahakama ilivyofafanua sheria hizo.
Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.
Kumeshuhudiwa maandamano ya wafuasi wa upinzani wanaopinga uchaguzi huo wa marudio na wanashinikiza maguezi ndani ya tume ya uchaguzi IEBC na pia katika mfumo wenyewe wa uchaguzi.
Click to see content: Kenya_provisional_results_ws_swahili
IEBC ilitangaza kwamba Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 ambayo ni asilimia 54.27 naye Bw Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74 katika uchaguzi huo wa tarehe 8 Agosti ambao matokeo yake yalifutwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...