BBC

Serikali ya Uingereza imependekeza mabadiliko makubwa katika uongozi wa shirika la utangazaji la BBC.


Katibu wa wizara ya utamaduni bwana John Whittingdale, anapendekeza idhaa ya BBC kuongozwa na bodi maalum ambayo itakuwa na wanachama waliochaguliwa na BBC yenyewe wala sio serikali.

Mabadiliko hayo hata hivyo yanaipa serikali nguvu zaidi jambo ambalo limetilia shaka uhuru wa BBC katika siku za usoni.

Fedha za kufadhili shughuli za idhaa hiyo kongwe zitalindwa na hata kuongezwa maradufu na serikali ya Uingereza.

Asilimia kubwa ya fedha zinazofadhili shughuli za BBC zinatokana na kodi inayotozwa kila mmiliki wa runinga nchini Uingereza.

Serikali imependekeza kuiongezea BBC takriban pauni milioni 300 kufikia mwaka wa 2020.

Ufadhili huo mkubwa unafuatia tathmini ya serikali inayotambua ushawishi mkubwa wa BBC kote duniani.

Mapendekezo mengine ni kama ifuatavyo

    Ruwaza mpya ya BBC: "kuzingatia maslahi ya umma katika kila jambo, kutopendelea upande wowote, kudumisha viwango vya juu vya habari zinazoelimisha kujuza na kutumbuiza wasikilizaji

    Bodi maalum kuchukua pahala pa wakfu iliyokuwa ikiiongoza BBC 

    BBC kuchagua wanachama wa bodi hiyo wala sio serikali

    Maamuzi ya Uhariri yatakuwa jukumu la mkurigenzi mkuu

    Ofcom kupewa mamlaka ya kuidhibiti BBC

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU