MTEULE THE BEST
Anna Mghwira
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, asubuhi hii ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) alipokaribishwa kuhutubia baada ya mkutano wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT) kufunguliwa rasmi na Rais John Magufuli mkoani Dodoma.
Mghwira, mwanasiasa shupavu aliyekuwa mwanachama wa chama cha ACT-WAZALENDO amesema baada ya kufanyakazi kama Mkuu wa Mkoa chini ya serikali ya Rais Magufuli, ameweza kuiona CCM inayobadilika ambapo sasa inaonekana wazi kuwa chama hicho kinakataa rushwa na kinaweka maslahi ya Taifa mbele.
Mghwira alikuwa ni mwanamke pekee aliyegombea kiti cha ufrais kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, uliomwingiza madarakani Rais John Magufuli
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha akimaanisha hajabaki mwenyewe.
Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma.
Akimjibu mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42, kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama wengi wa kutosha"
Hivi karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Alberto Msando na leo Anna Mghwira.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Lebo
TANZANIA
Lebo:
TANZANIA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni