Ronaldo atwaa tuzo ya Ballon D'or kwa mara ya tano
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo amemshinda mpinzani wake wa karibu Lionel Messi, katika tuzo hiyo na kuweza kuitwaa kwa mara ya tano na kuwa sawa na Messi ambae pia ametwaa kwa mara tano.
Nyota wa Barcelona Lionel Messi, amepata nafasi ya pili huku mchezaji mahiri wa Psg ya nchi Ufaransa Neymar Jr,akiwa katika nafasi ya tatu
Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012.
Ballon d'Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote
Maoni