Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Majaliwa aizungumzia Dar es salaam itakavyobaki baada ya Serikali kuhamia Dodoma

MTEULE THE BEST

Serikali imesema kwamba kuhamia Dodoma haiondoi hadhi ya Jiji la Dar es Salaam, na kwamba mji huo utabaki kuwa sehemu ya biashara.


Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akifungua ofisi ya Shirika la maendeleo ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa kuwepo kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma ni ishara ya kukamilika kwa serikali kuhamia rasmi mkoani humo.
"Leo nafungua ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Dodoma, zaidi ya watumishi 2376 wameshahamia Dodoma, mimi tayari nimehamia mapema, Makamu wa Rais Samia Suluhu ataungana nasi mwishoni mwa mwezi huu , mwakani tunategemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli atahamia huku", amesema Majaliwa.
Pia ameongeza kwa kusema, "Umoja wa Mataifa una mchango mkubwa sana katika Taifa letu, imechangia mipango mingi ya maendeleo , mpango wa kwanza ulianza mwaka 2011, wakati huu wa pili umeanza 2016 na utaishia 2021".
Aidha Majaliwa amesema hadhi ya mkoa wa Dar es salaam haitopungua ila itakuwa sehemu rasmi ya biashara.
"Viongozi kuhamia Dodoma hakuharibu hadhi ya mkoa huo, utabakia kuwa ni sehemu sahihi ya biashara, tunatengeneza njia sita ambazo zitatoka Ubungo hadi Chalinze, tunaimarisha mwendokasi ufike maeneo mengi pamoja na njia za reli iendayo haraka" , ameongeza Majaliwa.
Mpango wa kuhamia Dodoma ulianzishwa na aliyekuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1973, utekelezaji umeanza kufanyika mwaka 2017 ndani ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...