Italia yagongwa tena na tetemeko la ardhi

MTEULE THE BEST

Tetemeko laporomosha majumba Italia

Inasemekana kuwa watawa walinusurika kwa kukimbia kutoka ndani ya kanisa hili la mtakatifu Benedict mjini Norcia lililoporomoka
Image copyright@MONKSOFNORCIA
Image captionInasemekana kuwa watawa walinusurika kwa kukimbia kutoka ndani ya kanisa hili la mtakatifu Benedict mjini Norcia lililoporomoka
Tetemeko lingine baya la ardhi, limegonga maeneo ya katikati mwa Italia, mahali ambapo watu 300 waliuwawa mwezi Agosti mwaka huu.
Idara ya Seisomologia nchini Italia inakadiria kuwa tetemeko hilo lilikuwa lenye nguvu ya 6.5 katika vipimo vya Richa, tetemeko baya zaidi tangu lilile lililoitetemesha Italia mwaka 1980, iliyowauwa watu elfu 2,400.
Majumba yaliyonusurika tetemeko la Julya sasa yameporomokaImage copyrightSABRINA FATAUZZI
Image captionMajumba yaliyonusurika tetemeko la Julya sasa yameporomoka
Tetemeko la sasa limeporomosha jengo la kale la kanisa la mtakatifu Benedict mjini Norcia, pale wamonaki na watawa walikuwa wamekusanyika.
Meya wa mji ulioko karibu wa Ussita- Marco Rinaldi, amesema kuwa alikodolea macho kuzimu, kwani kila kitu kilichomzunguka kiliporomoka akitazama.
Barabara ya kuelekea Norcia imeharibiwaImage copyright@FRANC_PETRUCCI
Image captionBarabara ya kuelekea Norcia imeharibiwa
Duru zasema kuwa mji wa Amatrice -ambao uliharibiwa na tetemeko la mwezi Agosti, limeharibiwa tena zaidi.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kwamba watu tisa wamejeruhiwa lakini taarifa kuhusu vifo bado hazijatolewa.
Kitovu cha tetemeko hilo lilikuwa kusini mashariki mwa mji wa Perushia.
Maeneo ya Prague yatetemeshwa
Image capti

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU