MTEULE THE BEST
Marekani imendekeza vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwemo marufuku kwa biashara ya mafuta na kutwaliwa kwa mali ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Azimio lililowasilishwa kwa wanachama wa baraza la ulinzi wa Umoja wa Mataifa, linakuja baada ya jaribio la sita la nyuklia kufanywa na Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini inadai kuunda bomu la haidrojeni na imekwua ikitishia kuishambulia Marekani.
- Korea Kusini yafanya majaribio ya makombora kujibu majaribio ya Korea Kaskazini
- Bomu la Korea Kaskazini: Tunayoyajua kufikia sasa
China na Urusi zote zinatarajiwa kupinga vikwazo zaidi.
Korea Kaskazini tayari iko chini cha vikwazo vya kuitenga vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa, ambavyo vina nia ya kuulazimisha utawala wa nchi hiyo kusitisha mipango yake ya nyuklia.
Mwezi Agosti vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa vilipiga marufuku kuuzwa kwa mkaa wa mawe kutoka Korea Kaskazini ya thamani ya dola bilioni 1.
Pendekezo hilo la Umoja wa Mataifa linataka kuwekwa marufuku kabisa ya kuuzwa kwa bidhaa za mafuta kwenda Korea Kaskazini.
Pia pendekezo hilo linataka kutwaliwa kwa mali ya Bwa Kim na serikali ya Korea Kaskazini na pia kimpiga marufuku Kim mwenyewe na maafisa wengine wa vyeo vya juu kusafiri.
Wafanyakazi wa Korea Kaskazini nao watapiwa marufuku ya kufanya kazi nchi za kigeni.
- Korea Kaskazini yasifia jaribio jingine la nyuklia
- Bomu la Vita Vikuu vya Dunia lateguliwa Ujerumani
Pesa zinazotumwa nyumbani kutoka nchi za kigeni na mauzo ya bidhaa za nguo ndizo peke zilizobaki kuiletea fedha Korea Kaskazini
Lakini Marekani inatarajiwa kukabiliana upinzani kutoka China na Urusi ambazo zote huuza mafuta kwa Korea Kaskazini na zina kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa
Maoni