Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Bomu la Korea Kaskazini lilisababisha 'maporomoko ya ardhi'

MTEULE THE BESTPicture of landslides at Punggye-ri


Haki miliki ya pichaPLANET / 38 NORTH
Image captionPicha za 38 North zinaonesha maporomoko kadha yaliyokea karibu na kilele cha Mlima Mantap

Majaribio ya bomu la nyuklia ambayo yalifanywa na Korea Kaskazini Jumapili yalisababisha maporomoko kadha ya ardhi, kwa mujibu wa picha za setilaiti ambazo zinaaminika kuwa za kwanza kabisa za eneo ambalo majaribio hayo yalifanyika.
Majaribio hayo ya bomu yalifanyika chini ya ardhi katika eneo la kufanyia majaribio silaha linalotumiwa na Korea Kaskazini la Punggye-ri ambalo lina milima mingi.
Kundi la uchunguzi kwa jina 38 North limechapisha picha ambazo zinaonekana kuonyesha "maporomoko kadha katika eneo kubwa" kuliko yaliyowahi kushuhudiwa awali.
Mlipuko wa bomu hilo ulisababisha tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 kwenye vipimo vya Richter.
  • Tetemeko hilo lilisikika hadi China na katika baadhi ya maeneo ya Urusi.
    Korea Kaskazini imefanya majaribio sita ya silaha za nyuklia kufikia sasa, yote katika eneo la Punggye-ri, ambalo lina njia za chini kwa chini ambazo zimechimbwa ndani kwenye milima.
    Picha za karibuni zaidi za 38 North zilipigwa siku moja baada ya majaribio hayo kufanywa na zinaonesha maporomoko pamoja na maeneo yenye vifusi na matope.
    Kuna pia maeneo ya ardhi ambayo inaonekana yalirushwa juu angani lakini yakarejea tena chini bila kuhama.
    Picture showing the Punggye-ri test siteHaki miliki ya pichaPLANET / 38 NORTH
    Image captionPicha ya karibu katika eneo la majaribio ya silaha ya Punggye-ri iliyopigwa siku chache kabla ya jaribio la Jumapili...
    Picture of landslides at Punggye-riHaki miliki ya pichaPLANET / 38 NORTH
    Image caption...ukilinganisha na picha ya eneo hilo iliyopigwa Jumatatu.
    Uharibifu ulitokea karibu na Mlima Mantap, mlima mrefu zaidi eneo hilo la majaribio.
    Waliochunguza eneo hilo wamesema kulikuwa na "maporomoko makubwa na yaliyoenea sana kuliko tuliyoshuhudia wakati wa majaribio matano ya awali ambayo Korea Kaskazini iliyafanya."
    Lakini waliongeza kwamba ingawa tetemeko hilo lilisababisha tetemeko lenye nguvu sana, hakuna dalili kwamba njia ya chini kwa chini ambayo ilitumiwa kulipua bomu hilo iliporomoka.
    Baadhi ya wataalamu wanaamini kwamba mlipuko wa bomu ulisababisha shimo ambalo lilitumiwa kulipua bomu hilo Punggye-ri liliporomoka, sana kutokana na hali kwamba kulitokea tetemeko la pili mwendo wa dakika nane baada ya tetemeko la kwanza.
    Picture showing the Punggye-ri test siteHaki miliki ya pichaPLANET / 38 NORTH
    Image captionPicha ya Punggye-ri kabla ya majaribio inaonesha eneo hilo lilikuwa na miti, nyasi na majani...
    Picture of landslides at Punggye-riHaki miliki ya pichaPLANET / 38 NORTH
    Image captionLakini picha ya baada ya majaribio inaonesha maeneo ya milima hiyo yakiwa wazi, dalili kwamba kulitokea maporomoko ya ardhi
    Bomu la Jumapili linakadiriwa kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 50 na 120.
    Bomu la nguvu ya kilotani 50 linakadiriwa kuwa na nguvu mara tatu ukilinganisha na bomu la nyuklia lililoangushwa na Marekani katika mji wa Hiroshima mwaka 1945.
    Majaribio kufanywa eneo moja Korea Kaskazini yameibua wasiwasi kuhusu iwapo eneo hilo linaweza kuwa hatari, ingawa wataalamu wamegawanyika.
    Mapema wiki hii, wanasayansi wa China walieleza wasiwasi kwamba mlima huo unaweza kuporomoka na kutoa miali nururishi iwapo majaribio yataendelea kufanywa eneo hilo, gazeti la South China Morning Post liliripoti.
    Lakini shirika la 38 North awali lilikuwa limesema hakuna uwezekano wa majaribio hayo kusababisha mlipuko wa volkano katika milima hiyo.
    Marekani inaweza kuishambulia Korea Kaskazini?
    Mzozo huo umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, lakini hali kwamba Korea Kaskazini inakaribia kuwa na/ au tayari ina uwezo wa kuunda kichwa kidogo cha nyuklia kinachoweza kuwekwa kwenye makombora, na kwamba ina makombora yanayoweza kufikia Marekani bara, yanabadilisha mambo sana.
    Miezi kadha iliyopita, kumekuwa na hatua za 'uchokozi' mara kadha za Korea Kaskazini pamoja na majibizano kati yake na Marekani ambazo zimezidisha mzozo huo.
    Korea Kaskazini ilitishia kurusha mabomu karibu na kisiwa cha Guam ambacho kinamilikiwa na Marekani katika Bahari ya Pacific.
    Majuzinchi hiyo imerusha kombora kupitia anga ya Japan.
    Lakini huku majibizano yakiendelea, bado ni vigumu kubashiri ni nini kitafuata.
    Makombora
    Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
    Image captionUwezo wa makombora ya Korea Kaskazini

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...