MTEULE THE BEST
Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano na mabingwa wa Ligi kuu ya Hispania (La Liga), Real Madrid kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Alvaro Morata.
Inaelezwa kuwa uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 umegharimu takribani dola za kimarekani million 78 ambazo ni sawa na pauni milioni 60 za Uingereza.
Mapema leo, mchezaji huyo ambaye ni zao halisi la Real Madrid, ameagana na wachezaji wenzake wa Real Madrid akiwemo kocha Zinedine.
The Blues waliamua kuhamishia majeshi kwa Morata baada ya chaguo lao la awali Romelu Lukaku kuamua kuungana na Jose Mourinho katika kikosi chake cha Manchester United.
United na wenyewe walitajwa kumuhitaji Morata lakini walilazimika kugeukia wa Lukaku baada ya kushindwa kufikia dau lilotajwa kuwa ni dola za kimarekani milioni 97.
Maoni