Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TTCL PESA YAZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA

MTEULE THE BEST
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL Pesa uliofanyika Makamu Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam. 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba akimuonesha namna ya kutumia huduma ya TTCL Pesa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar Es Salaam. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua huduma mpya ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. Uzinduzi huo umefanyika katika Makao Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Omari Nundu ambaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya TTCL, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bwana Waziri Kindamba, Wajumbe wa Bodi  na wafanyakazi wa TTCL. 

Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Rais alisema uzinduzi wa huduma ya TTCL PESA ni mwendelezo wa jitihada za Kampuni hiyo kurejea katika nafasi yake ya awali ya kuwa suluhisho la kweli la utoaji huduma za Mawasiliano hapa nchini. 

ā€œKuzinduliwa kwa huduma hii ni uthibitisho mwingine kwamba, TTCL inatekeleza kikamilifu maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli ambaye ameelekeza kuwa,  Mashirika yote ya Umma yajiendeshe kwa faida, yatoe gawio Serikalini,  yawahudumie wananchi kwa kiwango cha juu kabisa cha ubora na kwa gharama nafuuā€ alisema Makamu wa Rais. 

Aidha, Makamu wa Rais alisisitiza kwamba TTCL PESA itawezesha wananchi kutuma na kutoa pesa kwa viwango vya chini kabisa kupita mitandao yote, pia itawezesha wananchi kulipia Bill za Umeme (LUKU), Maji, Vingā€™amuzi na kuwezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vya data vya TTCL.  Aliwataka TTCL  kuendelea kuwa wabunifu zaidi ili waweze kuongeza huduma nyingine kadiri mahitaji na siku zinavyokwenda. 

Akijibu kuhusu changamoto zilizotajwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Makamu wa Rais alisema Serikali inazijua na itaendelea kuzipatia majawabu. Hatahivyo aliwataka watumie vyema rasilimali walizopewa ikiwamo Mkongo wa Taifa na Kituo cha Kuhifadhia Kumbukumbu za kimtandao kupata pesa za kujiendeshea. 

Makamu wa Rais pia aliipongeza menejimenti ya TTCL kwa wazo lao la kufikiria kuanzisha kiwanda cha simu hapa nchini.  Alisema ā€œmsisitizo wa serikali yetu kwa sasa ni ujenzi wa uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025 kupitia uwekezaji katika viwanda hivyo wazo lenu la ujenzi wa kiwanda cha simu limekuja wakati muafakaā€. 

Mwisho, Makamu wa Rais alisema TTCL PESA itatoa fursa kubwa ya ajira kwa wananchi kuwa mawakala na  itarahisisha shughuli za kiuchumi hasa biashara na hivyo aliwasihi wananchi kuonesha uzalendo wao kwa kutumia huduma za TTCL.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...