MTEULE THE BEST
Mwelekezi na mwigizaji mashuhuri wa filamu Jackie Chan atapokea tuzo ya staha ya Oscar kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu.
Jopo linalotoa tuzo za Oscar pia limeidhinisha kutuzwa kwa mhariri Anne Coates, mwelekezi Lynn Stalmaster na mwandalizi wa filamu za makala Frederick Wiseman.
Rais wa jopo hilo Cheryl Boone Isaacs amewataja wanne hao kama "waasisi halisi na stadi katika kazi waliyoifanya".
Chan, 62, alikuwa mwigizaji nyota katika filamu nyingi za kung-fu zilizoandaliwa katika nchi yake ya kuzaliwa, Hong Kong.
Alivuma kimataifa kwa filamu kama vile Rumble in the Bronx, Rush Hour na filamu ya vibonzo ya Kung Fu Panda.
Maoni