Watanzania wawili mume na mke waliotambulika kwa majina ya Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa wamekamatwa na dawa za kulevya China katika uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou wakiwa na mtoto wao mdogo wa miaka 2 ambaye amerudishwa leo nchini Tanzania
Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Sheria za Madawa ya kulevya, Edwin Kakolaki amesema kuwa raia hao wa Tanzania Januari 19, 2018 uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda, Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82.
Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini, mtoto huyo amewasili leo nchini Tanzania na Serikali kusema kuwa watafanya utaratibu wa kuhakikisha wanawatafuta ndugu wa watu hao ili waweze kuwakabidhi mtoto huyo.
Aidha Kakolaki amewataka Watanzania kuendelea kuwaombea wazazi hao na kusema kuwa kwa sasa wanaendelea na mashtaka nchini China ambao wao mtu akikamatwa na madawa ya kulevya adhabu yao huwa ni kunyongwa tu.
"Tuna hakikisha kwamba huyu mtoto anapata ndugu zake ili aendelee kupata matunzo kama kawaida labda tu nipende kutoa wito kwa Watanzania wenzangu kwamba tumekuwa tunapiga vita sana biashara ya dawa za kulevya tunaomba watuelewe hii biashara kwa sasa haiwezekani, hebu fikiri hawa wanaokwenda China wana 'risk' maisha yao kiasi gani? Maanake ukienda China ukikamatwa hakuna kifungo kingine wala adhabu nyingine zaidi ya kunyongwa, tunaomba ujumbe huu uwafikie Watanzania na vijana wasidanganyike kwenda nchi za nje kwa ajili ya biashara za dawa za kulevya
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni