Spika wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema Demokrasia ya Wamarekani iko mashakani, rais anawaacha bila chaguo
Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi anasema bunge hilo litawasilisha mashtaka ya uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump, kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka yake.
"Demokrasia yetu iko mashakani, rais anatuacha bila chaguo la kufanya," alisema kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Democrat.
Ameyasema hayo siku moja baada ya kamati ya masuala ya sheria ya bunge kuanza kuangalia mashitaka yanayoweza kuwasilishwa dhidi ya rais huyo kutoka chama cha Republican.
Bwana Trump aliwaambia Wademokrats kama watataka kumshitaki basi waharakishe.
Alituma ujumbe wa Twitter muda mfupi kabla ya kauli za Bi Pelosi : " Kama mtanichunguza, mfanye sasa hivi, haraka, ili tuwe na kesi ya haki katika Seneti, ili nchi iweze kuendelea na shughuli za kawaida'':
Mbunge wa Congres jimbo la California, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi asunuhi kuwa " ushahidi si wa kuzozaniwa. Rais alikiuka mamlaka yake kwa ajili ya faida zake za kisiasa kwa kutumia usalama wa taifa letu , kwa kuzuwia msaada wa kijeshi na mikutano muhimu ya kitaifa ili kushinikiza uchunguzi ufanyike dhidi ya hasimu wake."
Aliongeza kuwa: "Tunatarajia kuwa na kesi ya usawa katika Seneti."
Mapema Alhamisi, mshauri wa ngazi ya juu ya Trump Kellyanne Conway aliwaambia waandishi wa habari : "Tuko tayari kwa kesi."
"Hapo ndipo upande wa utetezi utakapokika sheria," alisema, na kuongeza kuwa Republikan wanatarajia kuwaita mashahidi wao wenyewe.
Jumatano, Bi Pelosi alifanya mkutana wa faragha juu ya uchunguzi pamoja na Wademokrat wenzake na akawauliza : "Je mko tayari?"
Wabunge wakajibu kwa sauti ya juu "Ndio", kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press.
Jumatano , wataalamu wa sheria ya katiba walitoa ushahidi mbele ya kamati ya mahakama ya bunge kwamba vitendo vya Bwana Trump kutaka msaada kutoka kwa taifa la kigeni ni makosa ya kuchunguzwa.
Profesa wa nne alisema kuwavitendo vya Bwana Trump vilikuwa ni kosa, lakini si la kiwango cha kuchunguzwa.
Je inawezekana kumvua madaraka rais wa Marekani?
Trump anashutumiwa nini?
Katika mawasiliano ya simu, Trump alimtaka Bwana Zelensky amchunguze Joe Biden, ambaye kwa sasa ndiye mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine Burisma.
Uchunguzi unataka kubaini ikiwa Bwana Trump alitumia kitisho kuzuia msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuifanya imchunguze Biden na mwanae. Rais Trump amekana kufanya kosa lolote na ameutaja uchunguzi kuwa ni "hila".
Wiki iliyopita, Kamati ya masuala ya ujasusi ilikamilisha wiki mbili za kusikiliza kesi hiyo , kufuatia wiki kadhaa za vikao vya faragha ambapo waliwahoji mashahidi.
Adam Schiff, mwenyekiti wa kamati ya ujasusi, anayeongoza uchunguzi huo alisema kamati za masuala ya kigeni na intelijensia - ilitoa ripoti hiyo tarehe 3 Disemba.
Tutaendelea kukupatia maelezo zaidi juu ya taarifa hii...
Maoni