Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Menyekiti wa maswala ya fedha wa chama cha Republican tajiri Steve Wynn, ajiuzulu

Steve Wynn ni tajiri mkubwa wa biashara ya mchezo wa kamari Mchangishaji mkuu wa fedha za kisiasa wa chama tawala cha Republican, nchini Marekani, amejiuzulu wadhifa wake kwa sababu ya madai ya kuhusika na makosa kadhaa ya bughdha za ngono. Steve Wynn, bilionea mmoja mmiliki wa jumba la kuchezea kamari na rafiki mkubwa wa Rais Donald Trump, ametuhumiwa kwa kuhusika katika matendo kadhaa ya bughdha za kingono, dhidi ya wafanyikazi kadhaa wa kike. Kwa mjibu wa jarida la Wall Street, Wynn -- ambaye aliachia nafasi kama mwenyekiti wa kamati kuu ya kitaifa ya Chama cha Republican maswala ya kifedh-- wakati mmoja amewahi kumlipa mpambaji wake wa makucha mamilioni kadhaa ya dola, ili kuzima madai ya kumbughudhi kimapenzi mwanadada huyo. Steve Wynn na mkewe wa pili, Andrea Hissom, wakati wa kuapishwa kwa Rais Trump Amepuuzilia mbali madai hayo na kusema hayana msingi wowote. Anasema, mkewe wa zamani ambaye wangali wakizozana baada ya kutalikiana, ndiye aliyeanzisha u...

Daktari wa timu ya Olimpiki Marekani ahukumiwa kifungo

Larry Nasser daktari wa zamani wa timu ya Olympiki ya Marekani Aliyekuwa daktari wa timu ya Olimpiki Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo. Katika kesi hiyo mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa kumi. Alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria. Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine. 'Nataka ukae jela maisha yako yote'. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia. Muda mfupi baada ya kutolewa hukumu hiyo, mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nassar kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu...

Trump kukutana na rais Kagame wa Rwanda

Rais Trump alipokutana na baadhi ya viongozi wa bara Afrika katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mwaka jana Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa masuala ya kiuchumi World Economic Forum WEF unaofanyika mjini Davos , Uswizi. Bw Kagame atakuwa kiongozi wa pekee wa bara Afrika anayetarajiwa kukutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani H.R McMaster. Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa unajiri huku kukiwa na malalamishi makubwa dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika kuwa ''machafu" au ya "mabwege" katika mkutano wa kuzungumzia sera za uhamiaji. Baadaye alikana madai hayo. Mkutano wa rais Trump na Kagame, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na Marekani na kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo biashara na usalama. Rais wa Rwanda Paul Kagame kukutana na rais Trump katika mku...

Trump kukutana na rais Kagame wa Rwanda

Rais Trump alipokutana na baadhi ya viongozi wa bara Afrika katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mwaka jana Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa masuala ya kiuchumi World Economic Forum WEF unaofanyika mjini Davos , Uswizi. Bw Kagame atakuwa kiongozi wa pekee wa bara Afrika anayetarajiwa kukutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani H.R McMaster. Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa unajiri huku kukiwa na malalamishi makubwa dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika kuwa ''machafu" au ya "mabwege" katika mkutano wa kuzungumzia sera za uhamiaji. Baadaye alikana madai hayo. Mkutano wa rais Trump na Kagame, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na Marekani na kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo biashara na usalama. Rais wa Rwanda Paul Kagame kukutana na rais Trump katika mku...

Papa Francis: Majaribu ya 'nyoka' katika biblia ni kisa cha 'habari bandia'

Papa Francis Papa Francis ameshutumu njia za udanganyifu miongoni mwa wale wanaosambaza habari bandia akisema kuwa kisa cha kwanza cha habari bandia kipo katika biblia wakati Eve alipohadaiwa na nyoka kula tunda lililokatazwa. Kisa hicho kinaonyesha athari kali ambazo habari bandia zinaweza kusababisha, Papa Francis alionya katika nakala. Francis amesema kuwa hatua hiyo ilisababisha kusambaa kwa chuki na kiburi. Aliwataka watumizi wa mitandao ya kijamii na waandishi kutotumia njia ambazo zinaweza kusababisha migawanyiko. Nakala hiyo kwa jina Ukweli utakuwacha huru, habari bandia na uandishi wa amani ilitolewa kabla ya kufanyika kwa siku ya mawasiliano ya kanisa hilo itakayofanyika tarehe 13 mwezi Mei, na ilikuwa mara ya kwanza Papa Francis kuandika kuhusu mada hiyo. Amewataka watumizi wa mitandao ya kijamii na waandishi kukabiliana na njia za udanganyifu ambazo husababisha migawanyiko. Inajiri huku kukiwa na mjadala wa njia za kukabiliana na habari bandia ...

Hoteli ya Intercontinental Mjini Kabul yavamiwa na magaidi

Walinda usalama wa Afghanistan wamechukua udhibiti wa baadhi za ghorofa ya jumba hilo la Hoteli Msemaji wa Wizara ya usalama wa ndani nchini humo amesema kwamba, washambuliaji wawili kati ya wavamizi wanne, tayari wameuwawa. Yamkini watu 20 wanahofiwa kuwawa baada ya hoteli maarufu ya Intercontinental mjini Kabul, Afghanistan kushambuliwa na magaidi. Wanajeshi wa Afghanistan, wamekuwa wakipigana ghorofa baada ya ghorofa, ili kuchukua udhibiti wa hoteli moja ya kifahari katika mji mkuu Kabul, baada ya kuvamiwa na wapiganaji waliokuwa na silaha nzito nzito. Msemaji wa Wizara ya usalama wa ndani nchini humo amesema kwamba, washambuliaji wawili kati ya wavamizi wanne, tayari wameuwawa. Washambuliaji hao walivamia Hoteli ya Intercontinental jana Jumamosi jioni, na kuanza kuwamiminia risasi wageni na wafanyikazi pamoja na kurusha magruneti. Msemaji wa Wizara ya usalama wa ndani nchini humo, Nasrat Rahimi, ameiambia BBC kuwa, walinda usalama wamechukua udhibiti...

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 20.01.2018

Alexi Sanchez Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameorodheshwa miongoni mwa makocha wanaotarajiwa kumrithi Mkufunzi wa Chelsea Anonio Conte mwishoni mwa msimu huu huku aliyekuwa beki wa Cheslea Juliano Belletti akiwa mkurugenzi wa kandanda. (Star) Na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasakwa na klabu ya Paris St-Germain. (Mirror) Kiungo wa kati wa Brazil Malcom Tottenham inatarajiwa kuishinda Arsenal katika kumsajili mchezaji wa Brazil na Bordeaux mwenye umri wa miaka 20 Malcom. (Telegraph) Huenda mkataba haujaafikiwa lakini Mkufunzi wa Manchester Pep Guardiola ameipongeza Manchester United kwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez, 29. (Talksport) Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola Manchester City ilijiondoa katika harakati za kutaka kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal huku wakihofia kwamba hatua hiyo itaathiri vibaya udhabiti wa kifedha wa klabu hiyo.(Times - subscription required) Kiungo wa kati wa Ar...