Menyekiti wa maswala ya fedha wa chama cha Republican tajiri Steve Wynn, ajiuzulu


Steve Wynn ni tajiri mkubwa wa biashara ya mchezo wa kamari


Mchangishaji mkuu wa fedha za kisiasa wa chama tawala cha Republican, nchini Marekani, amejiuzulu wadhifa wake kwa sababu ya madai ya kuhusika na makosa kadhaa ya bughdha za ngono.


Steve Wynn, bilionea mmoja mmiliki wa jumba la kuchezea kamari na rafiki mkubwa wa Rais Donald Trump, ametuhumiwa kwa kuhusika katika matendo kadhaa ya bughdha za kingono, dhidi ya wafanyikazi kadhaa wa kike.


Kwa mjibu wa jarida la Wall Street, Wynn -- ambaye aliachia nafasi kama mwenyekiti wa kamati kuu ya kitaifa ya Chama cha Republican maswala ya kifedh-- wakati mmoja amewahi kumlipa mpambaji wake wa makucha mamilioni kadhaa ya dola, ili kuzima madai ya kumbughudhi kimapenzi mwanadada huyo.


Steve Wynn na mkewe wa pili, Andrea Hissom, wakati wa kuapishwa kwa Rais Trump


Amepuuzilia mbali madai hayo na kusema hayana msingi wowote.


Anasema, mkewe wa zamani ambaye wangali wakizozana baada ya kutalikiana, ndiye aliyeanzisha uzushi na uvumi huo dhidi yake


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU