Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

WATAMBUE WACHEZAJI 30WALIO CHAGULIWA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRICA

Walioteuliwa katika orodha hiyo ni: 1. Ali Maaloul (Tunisia na Al Ahly) 2. Bertrand Traore (Burkina Faso na Lyon) 3. Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal) 4. Christian Atsu (Ghana na Newcastle) 5. Christian Bassogog (Cameroon na Henan Jianye) 6. Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns) 7. Eric Bailly (Cote d'Ivoire na Manchester United) 8. Essam El Hadary (Egypt na Al Taawoun) 9. Fabrice Ondoa (Cameroon na Sevilla) 10. Fackson Kapumbu (Zambia na Zesco) 11. Jean Michel Seri (Cote d'Ivoire na Nice) 12. Junior Kabananga (DR Congo na Astana) 13. Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord) 14. Keita Balde (Senegal na Monaco) 15. Khalid Boutaib (Morocco na Yeni Malatyaspor) 16. Mbwana Samata (Tanzania na Genk) 17. Michael Olunga (Kenya na Girona) 18. Mohamed Salah (Egypt na Liverpool) 19. Moussa Marega (Mali na Porto) 20. Naby Keita (Guinea na RB Leipzig) 21. Percy Tau (South Africa na Mamelodi Sundowns) 22. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund) ...

CIA yatoa faili 470,000 za Osama Bin Laden

Shirika la ujasusi la Marekani CIA limetoa karibu faili 470,000 zilizopatikana wakati wa kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden mwaka 2011. Faili hizo mpya ni pamoja na stakabadhi kuhusu mipango yake binafsi na video ya mtoto wake wa kiume Hamza wakati wa hasuri yake. Marekani kumsaka mtoto wa Osama Makamando wa Marekani wavamia al-Qaeda Yemen Hii ndiyo mara ya nne CIA inatoa faili za Osama zilizopatikana wakati wa uvamizi kwenye maficho yake huko Abbottabad nchini Pakistan. Hata hivyo faili zingine haziwezi kutolewa kwa sababu zinaweza kuathiri usalama wa tiafa. Kulingana na CIA faili hizo zinafichua uhusiano uliopo sasa kati ya al-Qaeda na ISIS na migawanyiko kati ya al-Qaeda na washirika wake. Kampiuta iliyopataiaka wakati wa uvamizi huo ilikuwa na filamu za Hollywood, vipindi vya watoto na makala tatu kumhusu Osama Bin Laden. Mwana wa Osama bin Laden asakwa na Marekani Video nyingine ni ya harusi na mtoto wa Osama, Hamza Bin Laden akiwa mdogo. Hamza Bin...

Aliyetekeleza shambulizi la New York afikishwa mahakamani

Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamiaji kutoka nchini Uzbek anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani. Mshambuliaji awaua watu 8 kwa kuwagonga kwa gari New York Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kuwasambazia vifaa kundi la kigaidi la Islamic State. Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamaji kutoka nchini Uzbestan anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani. Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kusaidia kutoa vifaa kwa kundi la kigaidi la Islamic State. Akizungumzia mashataka yaliyofunguliwa kaimu mwanasheria mkuu JOON Kim amesema Saipov amefunguliwa mashitaka ya makosa mawili ya ugaidi. Shitaka la kwanza ni kutoa vifa vya kusaidia maandalizi ya shambulio la kigaidi kwa kundi la IS, na shitaka la pili kusababisha uharibifu wa magari...

SIO HABARI: SHILOLE

MTEULE THE BEST

Unbelievable Saves by David De Gea

MTEULE THE BEST

Makundi ya upinzani Syria yapinga mkutano wa amani uliofadhiliwa na Urusi

Licha ya Urusi kujitoa kudhamini mkutano wa amani ili kufikia makubaliano ya kisiasa kuhusu mgogoro wa Syria, wapinzani nchini humo wameukataa mkutano huo wakisisitiza ufanyike Geneva, chini ya Umoja wa Mataifa. Rais wa Urusi, Vladmir Putin Wakati huo huo, Waturuki wameuwekea mgomo mualiko wa Wasyria walio upande wa Wakurdi, huku juhudi hizo za kuleta amani zikikabiliwa na vikwazo siku ya Ijumaa. Licha ya kushiriki kimaamuzi katika vita vya Syria mwaka 2015 ikiwa upande wa Rais Bashar Al-Assad, Urusi sasa inaamini itajiimarisha kutokana na anguko la Dola la kiislamu IS, kwa kuzindua mchakato mpya wa kisiasa utakaopelekea kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miaka sita. Damascus imesema ipo tayari kuhudhuria mkutano wa Sochi utakaofanyika Novemba 18 ambao umepanga kuangazia katiba mpya na kusema kuwa ni wakati sahihi, shukrani kwa ushindi wa jeshi la Syria na kusambaratishwa kwa ugaidi. Lakini maafisa wa upande unaompinga Rais Assad, wameukataa mkutano huo na kusisitiza kuwa mazungu...

Viwango vya ajali vyashuka kwa asilimia 48 Tanzania

Viwango vya ajali vyashuka kwa asilimia 48 Tanzania Ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 48 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2017 ikilinganishwa na kipindi kama hicho 2016 kwa mujibu wa mkuu wa idara ya trafiki nchini Tanzania Fortunatus Musilimu. Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Kulingana na ripoti ya maafisa wa polisi, ajali za barabarani zilishuka kwa 1,264 ambayo ni asilimia 48. Hii ni kutoka 2,639 zilizorekodiwa 2016 hadi 1,375 mwaka huu. Kulingana na afisa huyo vifo na majeraha yalishuka kwa 239 ambayo ni asilimia 32 na 974 ambayo ni asilimi 40 mtawalia. Akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani, alisema kuwa kushuka kwa viwango hivyo kunatokana na juhudi za idara ya polisi wa trafiki, iliotilia mkazo sheria za trafiki mbali na kuhamasisha madereva na uma kuhusu sheria hizo. ''Tumekuwa tukitoa hamasa kupitia mipango kadhaa ikiwemo ule wa wiki ya usalama barabarani.Pia ninawaahidi kwamba nitaw...