Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Magufuli na Museveni waahidi kuimarisha ushirikiano

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao mbili. Wawili hao wamewaagiza Mawaziri wa nchi hizi mbili kujadiliana juu ya namna ya kuongeza biashara kati ya nchi hizo ili kupata manufaa makubwa zaidi ya uhusiano na ushirikiano uliopo. Dkt Magufuli na Bw Museveni walitoa agizo hilo baada ya kufanya mazungumzo rasmi katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda ambako Rais Magufuli ameendelea na ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku tatu. Rais Magufuli amesema kwa muda mrefu biashara kati ya Tanzania na Uganda imekuwa ni takribani shilingi Bilioni 200 kwa mwaka kiasi ambacho ni kidogo mno ikilinganishwa na fursa zilizopo, uhusiano na ushirikiano wa kidugu uliojengwa tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. "Tumewaagiza Mawaziri na wataalamu wakae na waangalie vikwazo vyote vinavyosababisha tufanye biashara kwa kiasi kidogo, wakishajadili watatuambia tufanye nini, tunataka kuona bias...

Korea Kaskazini: Trump anachafua amani duniani

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Korea Kaskazini imemuelezea Rais Trump kuwa mchafuzi wa amani na utulivu wa dunia, ambaye anatamani vita vya nuklia vitokee. Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Korea Kaskazini, imekariri nia ya taifa hilo kubaki na silaha zake za nuklia, ikisema silaha hizo zinalinda heshima na uhuru wa nchi. Matamshi hayo yanasadifiana na mazoezi makubwa ya manuwari za majeshi ya wanamaji, baina ya Marekani na Korea Kusini. Nduguye Kim Jong-un auawa Malaysia Nani alimrukia Kim Jong-un? Kim Jong-un aahidi kurusha makombora zaidi Pacific Hii ni mara ya kwanza katika mwongo mzima, ambapo manuwari tatu za Marekani zinazobeba ndege, kuhusika katika mazoezi hayo. Akiendelea na ziara yake katika bara la Asia, Rais Trump mara kadha, ameionya Korea Kaskazini, kwamba mradi wake wa silaha za nuklia, ni tishio ambalo halitovumiliwa.

Raia wa Korea Kaskazini aiomba China kutorudisha nyumbani familia yake

Raia mmoja wa Korea Kaskazini amemuomba rais wa China Xi Jinping kutomrudisha nyumbani mkewe na mwanawe wa kiume akisema kuwa watakabiliwa na kifungo jela au kifo iwapo watarudishwa Korea Kaskazini. Mwanamke na mvulana wa miaka minne wanaeleweka kuwa miongoni mwa kundi la watu 10 wa Korea Kaskazini waliozuiliwa nchini China wiki iliopita baada ya kuvuka na kuingia nchini humo kisiri. Mtu huyo ambaye alitaka kutambulika kwa jina la Lee pekee , alitorokea Korea Kusini 2015. Alirekodi ombi lake katika mkanda wa video ambao uliwasilishwa kwa BBC. Alisema kuwa mkewe na mwanawe watakabiliwa na hatia ya kifo ama kufungwa jela iwapo watarudishwa nyumbani Korea Kaskazini. ''Ningependa rais Xi Jinping na rais Donald Trump kumfikiria mwanangu kama kilembwekeza wao na kumleta mwanangu katika taifa huru la Korea Kusini '', alisema.tafadhali tusaidie. ''Okoa familia yangu kutorudishwa Korea Kaskazini. Mimi kama baba nawaomba viongozi hawa wawili kuisaidia familia yangu...

Trump na Putin 'waafikiana kuwashinda Islamic State nchini Syria

  State nchini Syria' Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamekubaliana kuhakikisha kundi la wapiganaji wanaojiita Islamic State (IS) wanashindwa nchini Syria, maafisa wa rais wa Urusi wamesema. Ikulu ya Urusi imesema taarifa imeandaliwa na wataalamu baada ya viongozi hao wawili kukutana kwa muda mfupi pambizoni mwa mkutano wa viongozi wa nchi za Asia na Pasific nchini Vietnam Jumamosi. Kwa jumla, viongozi hao wawili walikutana mara tatu katika kipindi cha saa 24 katika mji wa Da Nang. Hakujakuwa na thibitisho lolote rasmi kutoka kwa Marekani kuhusu tamko hilo la Urusi. Mkutano kati ya Rais Trump na Vladimir Putin ulitarajiwa kufanyika wakati wa mkutano huo wa Apec, lakini ni maelezo machache sana ambayo yametolewa. Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Julai katika mkutano wa G20 katika mji wa Hamburg nchini Ujerumani. Maswali kuhusu uhusiano wa Donald Trump na Urusi yamekuwa yakiulizwa mara kwa mara. Wasaidizi wake wakuu wa zamani wanachun...

Rais wa Ufaransa ziarani Saudi Arabia

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yuko nchini Saudi Arabia katika ziara isiyopanga, amesema atasisitizia umuhimu wa utulivu nchini Lebanon, katika mazungumzo yake na na viongozi wa nchi hiyo. Ufaransa ina uhusiano wa karibu na Lebanon, na ziara hiyo ya Rais Macron imekuja siku moja baada Waziri mkuu Saad Hariri, kujiuzulu wakati alipokuwa Riyadh, hali inayochochea hisia kwamba alishinikizwa na Saud Arabia. Awali akizungumza mjini Dubai, Rais Macron amesema anataka viongozi wa Lebanon kuishi huru ndani ya nchi yao. Amesema pia atautaka uongozi wa Saud Arabia kusaidia kuzuia baa la njaa nchini Yemen, ambako muungano wa majeshi yanayoongozwa na nchi hiyo yamefunga bandari kuzia silaha kuingizwa nchini humo na kuwafikia wapiganaji wa Ki Houthi.

Papa Francis apiga marufuku uuzaji wa sigara Vatican

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage caption Licha ya sigara kuiletea mamilioni ya fedha Vatican ,papa Francis amesema kuwa hawezi kuruhusu binaadamu kuathiriwa kiafya Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao. Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu. Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei . Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka. Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu. Mtoto amvua kofia Papa Francis Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka. ''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema. ''Ni kitu ambacho ni lazima...

Magufuli na Museveni waweka jiwe la msingi la bomba la mafuta Uganda

Image captionRais Museveni wa Uganda na Rais Magufuli walisaini mkataba wakuanza mradi wa bomba la mafuta ghafi mwezi Mei 2017 Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Rais hao wawili wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wakiwa katika kijiji cha Luzinga, jirani na mpaka wa Mutukula. Pia wamefungua kituo cha forodha chenye huduma zote muhimu kurahisisha safari kati ya nchi hizo mbili. Rais Magufuli anafanya ziara Uganda kwa siku tatu. Magufuli na Museveni wajadili bomba la mafuta Tamko la mradi wa bomba la mafuta ghafi lasainiwa Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima -Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu dola za marekani bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenz...