There are more than 545,018 miles of fibre cables under the sea - enough to wrap around the Earth almost 22 times Afisa wa cheo cha juu wa jeshi nchini Uingereza ameonya kuwa Urusi inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kwa uchumi ikiwa italenga nyaya za mawasiliano ya mitandao zinazopitia chini ya bahari. Sir Stuart Peach, mkuu wa majeshi, alisema kuwa nyanya hizo zinaweza kukatwa au kuharibiwa. Madai hayo yanazua maswali kadhaa: Hiki ni kitu Urusi inaweza kukifabnya? Ni kitu gani kitatokea ikiwa itafanya hivyo au ikiwa mtu mwingine atafanya hivyo? Nyaya hizo ni za kufanyia nini ? Zinatumiwa katika mawasiliano ya mitandao kati ya ya nchi tofauti na mabara. Nyaya zote hizo 428 zinachukua umbali wa kilomita milioni 1.1 na kuzunguka dunia nzima. Kiwango kikubwa cha data husambazwa kote duniani nchini ya bahari kwa nyaya na zingine hjuwa nyembamba kama karatasi. Je Urusi inaweza kukata nyaya za mawasiliano za chini ya bahari? Kwa bahati mbaya, huku teknoljia yao ikiwa ...