Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 01.01.2018

Eden Hazard Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 120 kwa mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Sun) Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekana kuwepo tofauti kati ya mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, na wachezaji wengine. (Sky Sports) Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, amekataa kukana kuwepo jitihada mpya kwa Sanchez baada ya Gabriel Jesus kupata jeraha wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili. (Talksport) Theo Walcott Southampton wanataka kumsaini wing'a wa Arsenal Theo Walcott 28, kwa mkono Januari hii. (Mail) Na Arsenal wanaweza kumuchia mchezaji huyo kuondoka huku Everton, Watford na West Ham wakiwa na dalili za kumsaini. (Mirror) Manchester United wanatumai kuwa kiungo wa kati Paul Pogba anaweza kumsaini mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 24, kujiunga na klabu hiyo. Joao Mario Naye meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kiungo wa kati wa Inter Milan Joao Mario 24, kuchukua mahala pake Mich...

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 31.12.2017

David Luiz Barcelona watatoa ofa ya pauni milioni 130 kumnunua Coutinho, 25, wiki hii, na wana uhakika kuwa watampata mchezaji huyo wa Liverpool ambaye walikosa kumnunua msimu uliopita. (Sunday Mirror) Arsenal wana nia ya kumsaini beki wa Chelsea David Luiz, lakini ikiwa Chelsea hawataki kuumuuza mchezaji huyo wa miaka 30 kwa mahasimu wao basi mbrazil huyo ataelekea Juventus. (Sunday Express) West Ham, wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle, 27, kutoka Borussia Dortmund. (Bild huko German) Emre Can Bayern Munich na Manchester City wanaaminiwa kujiunga katika mbio za kumpata kiungo wa kati wa Liverpol na Ujerumani Emre Can, 23. (Tuttosport - in Italian) Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema hajui mipango ya mshambuliaji Alexis Sanchez kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (Sunday Times) Ajenti wa Alexis Sanchez amezungumza na Manchester City kuwashawishi kumpa ofa ya mweze Januari mchezaji huyo ambaye anataka kuondoka Arsenal....

Rais mteule George Weah awataka raia wa Liberia walio nchi za kigeni kurudi nyumbani kuijenga nchi

Weah awataka raia wa Liberia walio nje kurudi kuijenga nchi Rais aliyechaguliwa nchini Liberia George Weah, amewashauri raia wa Liberia wanaoishi nchi za ng'ambo kurudi nyumbani ili kusaidia kuijenga nchi yao. Alitoa wito huo wakati wa mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu atangazwe mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia Nyota huyo wa zamani wa kandanda alisema ujuzi wa watu wa Liberia walio nchi za kigeni unahitajika kuijenga nchi hiyo. Bw. Weah alipongezwa aliposema kuwa ufisadi hautavumiliwa katika utawala wake. Anaingia madarakani rasmi mwezi Januari.

Rais Trump aishutumu China kwa kusafirisha mafuta Korea Kaskazini

Korea Kaskazini inahitaji mafuta lakini vikwazo vinazidi kuilemea Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amevunjwa moyo na China kufuatia ripoti kwamba iliruhusu mafuta kusafirishwa hadi nchini Korea Kaskazini . Katika Ujumbe wa twitter, bwana Trump alisema kuwa China ilionekana '' hadharani'' ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini . Amesema hakuwezi kuwa na suluhu ya kirafiki katika mgogoro wa Korea Kaskazini iwapo mafuta yataruhusiwa kusafirishwa hadi Pyongyang. China mapema ilikana kwamba kumekuwa na ukiukaji wowote wa azimio la Umoja wa mataifa la mafuta kati ya China na Korea Kaskazini . Wiki iliopita , Beijing iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90. Ujumbe wa twitter uliochapishwa na rais Donald Trump Vi...

George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia

MTEULE THE BEST George Weah Leo atangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo Mwanasoka maarufu George Weah ashinda urais Liberia George Weah Leo atatangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo baada ya kuongoza kwa asilimia 61.5 kati ya kura asilimia 98.1 zilizohesabiwa. Bwana Weah amemtangulia mpinzani wake Joseph Boakai kwa kura asilimia 60. Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hio kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia. baada ya matokeo kutangazwa. "Ninazielewa umuhimu na majukumu ya kazi kubwa niliyokabidhiwa leo. Mabadiliko yanakuja." George Weah ni nani? Weah ni mwanasoka maarufu aliyecheza kwenye klabu za soka za juu Ulaya kama Paris St-Germain (PSG) na AC Milan, kabla ya kumaliza taaluma yake nchini Uingereza kwa kuwachezea kwa muda mfupi klabu za Chelsea...

Babu Seya, Papii Kocha  KABLA YA KURUDI CONGO Kutoa shukurani RAIS Dkt. John Pombe Magufuli

Wasanii wa muziki wa dansi Nguza Viking 'Babu Seya' na mwanawe Johnson Nguza 'Papii Kocha' ambao kwa sasa wapo mapumzikoni wanahangaika kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili waweze kumshukuru. Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini Mzee King Kiki amefunguka na kusema kuwa wasanii hao Babu Seya na Papii Kocha kwa sasa wapo mapumzikoni na kuwa wanahangaika kupata nafasi ya kuonana na Rais ili waweze kumshukuru kutokana na kuweza kuwapa msamaha mnamo Disemba 9, 2017 uliowafanya kuwa huru baada ya kutumikia jela kwa zaidi ya miaka 10.  "Saizi Nguza na Papii wapo kwenye mapumziko lakini wanapaswa kurudi nyumbani Congo kwenda kutekeleza mambo ya kimila, hivyo hawapaswi kufanya jambo lolote lile kwa sasa mpaka wakamilishe hilo suala la kimila, ila kabla ya wao kuondoka tumekuwa tukiomba kama tunaweza kupewa nafasi ya kuonana na Mhe. Rais kumshukuru na kumpa ahsante itakuwa ni vizuri...

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 28.12.2017

MTEULE THE BEST Mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Antoine Griezmann. (Marca) Manchester United haitashindana na Barcelona katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Antoine Griezmann. (Marca) Paris St-Germain wanachunguza hali ya Marouane Fellaini katika uwanja wa Old Trafford na wako tayari kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 katika uhamisho wa bure msimu ujao.(Daily Mirror) Liverpool ilimsafirisha daktari wake ili kuchunguza hali ya kimatibabu ya beki wa Southampton , 26, Virgil van Dijk ili kuweza kukamilisha usajili wa dau la £75m haraka iwezekanavyo - kabla ya Mancity kuwa na hamu ya mchezaji huyo .(Liverpool Echo) Yannick Carrasco, 24, katika dirisha ka uhamisho la mwezi Januari(AS) Atletico Madrid wanafurahia kumuuza winga Yannick Carrasco, 24, katika dirisha ka uhamisho la mwezi Januari(AS) Chelsea ilifeli katika harakati za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Ubelgiji msimu uliopita lakini ...