Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Rais George H.W. Bush afarikia dunia

Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W. Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 huko mjini Houston, msemaji wake Jim McGrath amethibitisha kifo chake. George H.W. Bush Rais huyo wa zamani wa Marekani aliongoza kwa awamu moja tu akiingia madarakani mwaka 1989 na kuondoka 1993 hivyo kubaki kama Rais pekee aliyeiongoza Marekani kwa awamu moja. Chanzo cha kifo cha George Bush hakijawekwa wazi rasmi, lakini Rais huyo mstaafu wa Marekani, kwa muda mrefu alikuwa akipambana na ugonjwa wa 'Vascular Parkinsonism', na kifo chake kimetokea ikiwa imepita miezi michache tangu mke wake Barbara Bush afariki dunia mnamo April 17, 2018 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taarifa zaidi zinasema kwamba George Bush alikumbwa na ugonjwa huo tangu miaka ya 90, na mwenyewe aliwahi kuulezea kuwa ni ugonjwa mzuri kuupata kwani haumuumizi, isipokuwa tu anashindwa ku-'move' pale anapotaka hata kunyanyua mguu.  "Unaathiri miguu, hauumii, unaiambia miguu yako ijongee na haijon...

Vicensia Shule: Aliyekuwa na ujumbe wa Magufuli aitwa kamati ya maadili

Dkt Vicensia Shule anasema ulinzi wa Dkt Magufuli ulimfanya anyamae Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyezua mjadala mtandaoni baada ya kudai kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni humo ameitwa kufika kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho. Barua ya kamati hiyo iliyotiwa saini ya mwenyekiti Prof Evelyne Mbede inamtaka mhadhiri huyo kufika mbele ya kamati hiso Ijumaa saa tisa "ili kamati iweze kulifanyia kazi swala hili kwa haraka." Dkt Vicensia Shule alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba alitaka sana kuufikisha ujumbe wake kwa Rais John Magufuli lakini aliwaogopa walinzi wake. Dkt Magufuli alikuwa amezuru chuo hicho kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) jijini Dar es Salaam. Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati ilijengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo Ch...

Diamond hatimaye hapata mpenzi mpya

Tanasha Donna Oketch: Mkenya huyu 'anayependwa' na mwanamuziki Diamond Platnumz ni nani hasa? Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz ametangaza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba yuko katika uhusiano wa kimapenzi na Mkenya, au si uhusiano? Platnumz amepakia video kuashiria kwamba yuko kwenye mahaba na dada kwa jina Tanasha Donna Oketch. Bi Oketch, ni mtangazaji katika kituo cha redio cha NRG nchini Kenya. NRG ni miongoni mwa vituo vipya vya redio nchini Kenya ambavyo vimekuwa vikilenga kuwavutia zaidi vijana. Diamond, ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul Juma, kwenye video ya Insta Stories Jumanne aliandika kuwa: "Maskini simba yuko kwenye mapenzi…Mmwamini, yupo kwenye mapenzi." Mwanamuziki huyo kwa utani hujiita Simba au Chibu Dangote. Video inayoonyesha vivuli vya wanaoaminika kuwa yeye na Tanasha wakitembea ufukweni inaonesha ujumbe wa "I love you Tanasha" (Nakupenda Tanasha) ambayo yameandikwa mchangani. Diamond, ambay...

Kabakama - mchezaji wa mchezo nchini Tanzania

mteulethebest Jeremia Rukya Kabakama ni mmoja wa wanawake wa kwanza wa Afrika wanaofanana na viongozi na kwa sasa ni katika Kombe la Mataifa ya Wanawake ya Jumla ya Wanawake Ghana 2018. Huu ndio kuonekana kwake kwa pili katika ushindani wa wanawake wa baraza, na hadi sasa amesimama mechi mbili; Mali vs Cameroon (kikundi cha hatua) na Afrika Kusini vs Mali (nusu ya mwisho). Katika nchi yake ya asili ya Tanzania, yeye anajulikana sana kwa kutangaza derby kubwa katika nchi ya Mashariki mwa Afrika, kati ya wapinzani wa milele Young Africans na Simba, ambayo pia inahesabu kati ya wengi waliyosema juu ya bara. Na yeye amefanya si mara moja lakini mara tatu, na wote bila ya utata. Alizaliwa huko Kagera, sehemu ya kaskazini-magharibi mwa Tanzania, CAFOnline.com ilipata naye kumwambia hadithi yake na kushiriki uzoefu wake kama Upepo wa Wanawake wa Umoja wa Mataifa Ghana 2018. Chini ni vifungu; Cafonline.com: Ni wakati gani na jinsi gani umekuwa mwamuzi? Jeremia Rukya Kabakama: Il...

Sababu zilizochangia benki tano kupigwa marufuku ya kubadilisha fedha za kigeni Tanzania

Noti za Tanzania Benki Kuu ya Tanzania imezipiga benki tano marufuku ya kuendesha biashara ya sarafu za kigeni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukiuka sheria kwa mujibu wa maafisa wa vyeo vya juu. Marufuku hiyo inakuja baada ya Benki Kuu kufanya ukaguzi wa ghafla kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwenye mji ulio kaskazini wa Arusha kituo cha utalii na bishara ya madini. Kwa sasa kuna zaidi ya benki 40 zinazotoa huduma kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Kwa nini zimepigwa marufuku? Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara, kwa mujibu wa Alexander Ng'winamila, mkurugenzi wa masoko ya fedha katika benki kuu. "Benki zilizopigwa marufuku aidha zilifanya biashara nje ya viwango vya masoko au hazikuwasilisha kwa Benki Kuu rrekodi za biashara zao, suala ambalo ni kinyume na sheria," Ng'winamila aliliambia shirika la Reuters. Barc...

Makamu wa Rais akutana na Mabalozi wa Palestina na Japan Ikulu

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amekutana na Balozi wa Palestina pamoja na Balozi wa Japan jijini Dar es salaam.    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam

Simba yaicharaza Mbabane Swallows FC Kipigo cha mbwakoko

Timu ya Simba imeanza vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwakuapiga Mbabane Swallows FC 4-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.  Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane.  Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1.  Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.  Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza