Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana furaha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii Alikuwa ni mtu aliyependa sherehe kubwa ambazo zilikuwa zikiandaliwa mara kwa mara na chama tawala cha Zanu-PF Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana raha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii baada ya kutawala kwa miaka thelathini na saba. Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kwamba alimtembelea mjombake ambaye anasema anaendelea vizuri baada ya utimuliwa kwake madarakani. Kauli ya Leo Mugabe inaashiria kiongozi huyo mkongwe amezoea kwa upesi kutimuliwa kwake kutoka uongoai wa taifa hilo. Amesema mjombake anatazamia maisha yake ya baada ya uongozi, ambayo yatajumuisha ukulima na kuishi katika nyumba yake mashambani. 'Grace, bado yupo naye' amesema Leo Mugabe akimaanisha mkewe rais huyo wa zamani. Ameeleza kuwa anashughulika na mipango ya kujenga chuo kikuu kwa heshima ya m...