Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Rais Trump ayatusi mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador

Rais Trump ameyatusi mataifa ya Afrika , haiti na El salvador akidai ni machafu Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse. ''Kwa nini tunawaruhusu watu hawa kutoka mataifa 'machafu''?. Rais Trump aliwaambia wabunge siku ya Alhamisi kulingana na gazeti la The Washington Post. Tamko hilo lilidaiwa kuwalenga watu kutoka Afrika, Haiti na El Salvador. Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari. ''Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa M arekani pekee,taarifa iliotoka katika msemaji wa Ikulu Raj Sha ilisema. Iliendelea: Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu ...

Sababu ya Ronaldo kuorodheshwa wa 49 duniani

Ronaldo, atakuwa na miaka 33 mwaka huu, na alitawazwa mchezaji bora duniani miaka 4 kati ya tano iliyopita Cristiano Ronaldo amefunga mabao 58 miaka miwili iliyopita na kuwasaidia Real Madrid kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili mtawalia na pia La Liga mara moja. Miaka hiyo miwili iliyopita, ameshinda tuzo ya mchezaji bora duniani, tuzo ya Ballon D'Or, mtawalia. Anafaa basi kuwa mchezaji bora zaidi duniani na thamani yake kuwa ya juu zaidi? Ni kweli uchezaji wake hauna kifani. Lakini kwa thamani, la hasha. Utafiti huo wa shirika la takwimu za michezo la CIES Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la takwimu za michezo la CIES iliyotolewa Jumatano, mchezaji huyo ni wa 49 kwa thamani duniani. Anayeongoza orodha hiyo ni mshambuliaji wa Paris St-Germain ya Ufaransa, Mbrazil Neymar, 25, ambaye ndiye mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na klabu yoyote duniani na mwenzake wa Barcelona Lionel Messi, 30, kutoka Argentina. Mshambuliaji wa To...

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 11.01.2018

Winga wa Arsenal Theo Walcot Everton imejiunga na vilabu vilivyo na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot 28. Muingereza huyo pia anasakwa na klabu yake ya zamani Southampton huku Arsenal ikidaiwa kutaka dau la £30m. (Liverpool Echo) Mchezaji wa RB Leipzig na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita huenda akajiunga na Liverpool mwezi huu. Mchezaji wa RB Leipzig na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita huenda akajiunga na Liverpool mwezi huu. Liverpool tayari wamemsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa dau la £48m lakini wanaweza kulipa kati ya Yuro milioni 15-20 ili kumchukua kabisa.(Bild - in German) Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill alitarajiwa kukutana na maafisa wa klabu ya Stoke siku ya Jumatano kuhusiana na wadhfa wa mkufunzi ulio wazi huku naibu wake Roy Keane pia akitarajiwa kuondoka iwapo atachukua wadhfa huo. (Irish Independent) Guangzh...

Meli yenye bendera ya Tanzania yanaswa Ugiriki

Mwaka 2016, Tanzania ilifutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria Maafisa wa Ugiriki wanaoshika doria baharini wamesema wanaizuilia meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ambayo ilikuwa imebeba vilipuzi. Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya. Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi ikiwemo. "Maafisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," afisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki Yiannis Sotiriou aliwaambia wanahabari, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ANA. Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikendi baada ya maafisa kupashwa habari na mdokezi. Ilisindikizwa hadi katika bandari moja kisiwa h...

Arsene Wenger amlilia Alexis Sanchez kusalia Arsenal

Sanchez anahusishwa na uhamisho wa Manchester City mwezi huu. Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa uamuzi wake wa kumchezesha Alexis Sanchez kama mchezaji wa ziada dhidi ya Chelsea siku ya Jumatano hauna uhusiano na uvumi kuhusu uhamisho wake na kusisitiza hamu yake ya mshambuliaji huyo kusalia katika kabu hiyo. Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye kandarasi yake inakamilika mwezi Juni aliingia katika kipindi cha pili katika nusu fainali ya kombe la Carabao mkondo wa kwanza mbapo timu hizo zilitokare sare tasa. Sanchez anahusishwa na uhamisho wa Manchester City mwezi huu. ''Nataka asalie kwa kipindi kirefu'',alisema Wenger. ''Sina tatizo iwapo atasaini kandarasi mpya nasi iwe sasa au mwezi Juni''. Lazima ukubali wakati unapocheza mechi nyingi na Sanchez hucheza kila mechi, na kwamba wanapopimzika katikati ya msimu huwasaidia kidogo. Licha ya utata unaokumba hatma ya Sanchez, Wenger haamini kwamba Sanchez anataka kuondoka....

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.01.2017

Alexis Sanchez Manchester City wameipatia Arsenal dau la £20m ili kumsajili Alexis Sanchez, 29, huku mshambuliaji huyo wa Chile akidaiwa kukubali malipo ya £250,00 kwa wiki..(Guardian) Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anatarajiwa kuilipa Boca Juniors kitita cha pauni milioni 27 kumsajili Cristian Pavonkatikaligi Premia. (TyC Sports - in Spanish) Wakati huohuo, Wenger anatarajiwa kukaa katika viti vya mashabiki katika uwanja wa Stamford Bridge kwa mechi ya Jumatano ya nusu fainali ya kombe la carabao baada ya kupigwas marufuku ya kukaa katika eneo la wakufunzi (Express) Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hataki kuwasajili wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho licha ya kuwa nyuma ya viongozi wa ligi ya La Liga Barcelona.. (Reuters) Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaondoka Old Trafford kabla ya kukamilika kwa msimu huu. Raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 36 hana kandarasi na klabu hiyo. (Yahoo Spo...

Hatari tano kwa biashara Afrika Mashariki 2018

Kenya inarudi katika hali ya utulivu kisiasa baada ya uchaguzi wa rais uliochukua muda mrefu na uliokumbwa na misukosuko. Hata hivyo changamoto zitaendelea kuwepo mwaka huu kwa mashirika yanayohudumu nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kitaalamu Control Risks linalochambua hatari na udhibiti wa hatari za kibiashara na uwekezaji. Daniel Heal ambaye ni mshirika mkuu wa shirika hilo katika kanda ya Afrika Mashariki, amesema "mwaka 2018 ni mwaka wenye matumaini kwa Kenya na Afrika Mashariki. Tayari tumeanza kuona imani ya wawekezaji ikirejea taratibu kufuatia udhibiti wa kisasa Kenya na azma katika miradi mipya ya miundo mbinu Kenya na katika kanda hiyo kwa jumla. Tunatarajia hili kuendelea hadi mwisho wa mwaka huu." Hata hivyo Daniel anasema nchini Kenya, hitaji la kulipa awamu ya kwanza ya mkopo wa fedha za Eurobond ambazo zilikuwa dola milioni 774.8, linapaswa kuishawishi serikali kudhibiti ukopaji na matumizi kabla deni kufi...