Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Serikali yawahakikishia wananchi upatikanaji maji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha wananchi katika vijiji vyote nchini wanapata huduma ya safi na salama wakiwemo na wa jimbo la Bumbuli. Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Mhandisi wa Maji wa Halmashauri  ya Bumbuli, wilayani Lushoto, Charles  Boy afanye utafiti na kubainisha vijiji vyenye shida ya maji Bumbuli. Amesema baada ya kuvibaini vijiji hivyo, anatakiwa aweke mpango wa kuhakikisha navyo vinapata huduma ya maji safi ili kuwaondolea wananchi tatizo hilo la ukosefu wa  maji. Alitoa agizo hilo Alhamisi, Novemba 1, 2018 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mponde jimbo la Bumbuli, Lushoto. Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, aliwapongeza wakazi wa wilaya ya Lushoto kwa kutunza mazingira na vyanzo vya maji. Alisema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye c...

RC Arusha aonya wakandarasi wababaishaji

RC ARUSHA AONYA WAKANDARASI WABABAISHAJI  Na Ferdinand Shayo,Arusha.  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo ameonya Wakandarasi wanaofanya ubabaishaji kwenye miradi ya barabara za vijijini Mkoani Arusha kwa kutopewa tenda za serikali na badala yake wachukuliwe hatua za kisheria.  Gambo ametangaza marufuku kwa wakandarasi wababaishaji kupewa kandarasi  wakati akikabidhi mikataba ya kwa   wakandarasi wa wilaya za saba za mkoa wa Arusha ikiwemo Arusha,Meru na Karatu .  Aidha amewataka Wakandarasi kuhakikisha kuwa wanakamilisha miradi kwa wakati na kutumia vizuri fedha za walipa kodi na kuepuka kutekeleza miradi chini ya kiwango.  Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Richard Kwitega amesema kuwa serikali imewapa kipaumbele Wakandarasi wazawa ili waweze kuleta tija kwenye miradi ya Barabara ambazo zitachochea maendeleo ya wananchi.  Kaimu Mratibu wa Tarura mkoa wa Arusha Dickson Kanyankole  amesema kuwa miradi hiyo itatekelezwa ka...

Ndege mpya inawezaje kuanguka

Lion Air: Haki miliki ya pichaBOEINGImage captionNdege aina ya Boeing MAX 8 ilikuwa imehudumu chini ya mwaka mmoja Ndege ya shirika la Lion Air iliyoanguka baharini, ikiwa na abiria karibu 190 muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu wa Jakarta nchini Indonesia imeendelea kuvutia hisia mbali mbali. Ndege hiyo aina ya Boeng 737 MAX 8, ilikua mpya. Hii ni ajali ya kwanza kuhusisha ndege aina hiyo. Maelezo kuhusu nini hasa kilitokea yamekua finyu lakini chanzo cha ajali hiyo kitajulikana baaada ya uchunguzi kufanywa. Ajali ya ndege mara nyingi husababishwa na mchanganyiko wa mambo tofauti ikiwa ni pamoja na hitilafu ya kimitambo au makosa ya kibinadamu-lakini je ndege mpya inawezaje kuanguka? Ndege hiyo ya Boeng 737 MAX 8 iliyohusika katika ajali siku ya jumatatu ilikuwa imehudumu kutoka mwaka Agosti 15 mwaka 2017 Kwa mujibu wa mkuu wa tume ya kitaifa ya usalama wa uchukuzi wa angani Soerjanto Tjahjano ndege hiyo ilikua imesafiri kwa saa 800. Inasemekana rubani aliomba w...

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 30.10.2018

: Mauricio Pochettino, Antonio Conte, Loris Karius, Divock Origi, Jose Mourinho, Ousmane Dembele, Cristiano Ronaldo Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express) Real Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na Barcelona Jumapili. (Sun) Mazungumzo ya Real na kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ya kumtaka achukue mikoba ya ukufunzi Madrid yamekwama. Hii ndiyo sababu iliyochangia Santiago Solari ambaye ni mkufunzi wa timu ya akiba kuwekwa kwenye usukani. Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ni miongoni mwa wanaopigiwa u...

Bilioni 20 za Mo kwa Simba zapangiwa matumizi

Mohammed Dewji ambaye ni mmiliki wa asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba. Mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba Swed Mkwabi, ameweka wazi mipango yake na kuomba wanachama wa klabu hiyo wamchague.  Kampeni za uchaguzi huo wa Simba utakaofanyika November 4, 2018, zimefunguliwa rasmi jana, na leo Mkwabi ameweka wazi mipango yake kwa kusema atahakikisha pesa ya uwekezaji bilioni 20 itakayotolewa na Mohammed Dewji inaongezeka maradufu.  ''Bilioni 20 ni pesa nyingi lakini inahitaji weledi mkubwa wa kuifanya endelevu, inaweza ikachotwa ndani ya miaka mitatu ikaisha tukashindwa kuzalisha tena tukarudi tulikotoka kwa hiyo kama nitapata fursa kwa kushirikiana na wenzangu tutatengeneza misingi ya kibiashara kuitoa katika bilioni 20 kuifanya iwe zaidi'', ameeleza.  Aidha Mkwabi amesema kuwa ameshagundua wanachama wa Simba wanataka wajumbe wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa ajili ya Simba na anaamini wanajua kuchuja mjumbe gani anafaa na yupi hafai hivyo hat...

Namna ya kuachana kwa amani na mpenzi wako

MAPENZI Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:  1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya:  Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya ku...

Daraja refu zaidi duniani

mteulethebest Daraja refu zaidi duniani linalounganisha Hong Kong-Zhuhai China litafunguliwa rasmi hapo kesho. Daraja hilo lenye umbali wa kilomita 55km  limegharimu takriban dola bilioni $20 za Marekani. Ujenzi  ulianza mwaka wa 2009. Safari ya kawaida kati ya China na Hong Kong ilikuwa inachukua muda wa takriban saa 4. Daraja hili linapunguza muda huo wa usafiri hadi dakika 30 pekee. Je nini kinaizuia Afrika isipige hatua ya maendeleo  kama hii?