Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Benki ya Dunia yamwaga Tanzania shilingi Bilioni 680.5 za utekelezaji miradi ya maendeleo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na shilingi Bilioni 680.5 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari unaokusudiwa kujenga vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, nyumba za watumishi na kununua vifaa vya kufundishia.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem Ikulu jijini Dar es Salaam aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es SalaamMakamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem aliyekutana na Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 16 Novemba, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema pamoja na kuridhia kutoa fedha za mradi huo, Benki hiyo inaendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nch...

Mwaka mchungu na mtamu kwa Diamond

Toka mwaka 2009 hadi sasa Diamond Platnumz amekuwa akifanya vizuri kimuziki na kipindi chote hicho ameweza kushinda tuzo za ndani na za kimataifa pia. Kabati lake lina tuzo kubwa zaidi ya 10 kama Channel O Music Video Awards, HiPipo Music Awards, MTV Europe Music Awards/WORLDWIDE ACT AFRICA/INDIA, MTV Africa Music Awards, African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) na nyinginezo.  Kwa mwaka huu amefanya mengi makubwa na mazuri ingawa amekuwa na changamoto kubwa kwake.Chini nimeweka yale aliyofanikiwa na yale yalimpatia changamoto kwa huu.  1. Muziki Wake   Ni mwaka ambao Diamond Platnumz amejikuta nyimbo zake tatu zikifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Diamond hakuwa msanii wa kufungiwa lakini mwaka huu upepo huo umempuliza vilivyo.  February 28, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo ni zile ambazo hazikupaswa kuchezwa kwenye vyombo vya habari....

Maneno ya Manara kwa Rostam 'Ukiingia Yanga unaanza kulipa madeni kama yote'

Baada ya Rostam Aziz kusema yeye ni shabiki wa timu ya mpira ya Yanga alipoulizwa na Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.  Hatimaye Msemaji wa timu ya Simba,  Haji Manara amemuomba Rostam kuisaidia timu ya Yanga.  Manara kupitia ukarasa wake wa Instagram amesema kuwa Yanga walivyo na njaa akiingia ataanza kulipa madeni kama yote na mishahara.  "Sasa Shekh Rostam kwa kuwa umedeclere leo mbele ya bwana mkubwa kuwa ww ni Yanga na hali zao ni taabani sana kiasi cha kumlilia mtu aendelee kuwaongoza!! Hebu njoo huku kwenye mpira basi, au ww Yanga jina tu," aliandika Manara.  Aliongeza "Na walivyo na njaa ukiingia tu unaanza kulipa madeni kama yote na mishahara!!  Nategemea povu la kufa mtu toka Mbuteni."

Lulu Amaliza Rasmi Kifungo Chake

Mwanadada Elizabeth Michael amemaliza rasmi kifungo chake alichokuwa akitumikia kwa muda saa akiwa nje na November 12 ndio ilitakiwa kuwa huru kwa kukimaliza kifungo hicho.  Mwanadada Lulu ambae alikuwa nje akitumia kifungo cha nje huku akipangi wa kufanya kazi mbalimbali za kijamii amekuwa huru kuanzia sasa na kwamba hata zile kazi alizokuwa akifanya za kijamii itakuwa zimefika kikomoe kuanzia sasa.  Lulu alihukumiwa kifungo cha jela baada ya kukitwa na kesi ya kuua bila kukusudia kwa mwanamaigizo mwenzake Steven Kanumba mabae alikuwa ni mpenzi wake pia walipokuwa wakikorofisha  na kumsukuma kwa bahati mbaya na kuuumia sehemu za kichwa.  Mwanadada Lulu anaingia uraia tena akiwa tayari amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi Majizo ambao walitangaza ndoa hiv karibuni

Tambua njia za kufuata kuleta suluhu za mifarakano katika mahusiano

Migongano na tofauti kati ya watu wawili katika mahusiano ni kitu kisichoepukika iwe ni mahusiano ya mapenzi ,mahusiano ya mzazi na mtoto na hata mahala pa kazi. Sababu za mifarakano katika mahusiano ziko wazi;kwamba watu hawa wametoka na kukulia katikla mazingira tofauti na hivyo tabia na hulka zao ni lazima zitatofautiana.  Katika hali kama hii migongano na kutoelewana wakati mwingine ni vitu ambavyo vinatokea na kunahitajika busara na mbinu mahususi za kukabiliana na tatizo hili  Njia 7 Muhimu za Kutatua Mifarakano Katika Mahusiano   1. Kuwa wa Kwanza Kuchukua Hatua   Kunapotokea kufarakana kati ya watu wawili kwa kawaida mawasiliano huvunjika au kuwa magumu na mabaya. Kila mmoja anaweza akwa na kinyongo na mwingine. Kwa wapenzi hali hii inaweza ikawa ya kuumiza zaidi kwani inahusisha hisia kwa kiasi kikubwa;ni jukumu lako wewe kufunja ukimya na kuwa wakwanza kuleta suluhu.  Tafuta nafasi na omba kujadili na kuongea kuhusu tofauti zenu.  2. An...

Mama Samia aionya Takukuru kukumbatia wala rushwa

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameionya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Rombo kutokana na taarifa kwamba baadhi ya maofisa wake wanatumika kuwalinda watendaji wa serikali wanaojihusisha na rushwa.  Samia alitoa onyo hilo jana akiwa katika sehemu ya ziara yake ya siku tano ya kikazi mkoani Kilimanjaro.  Alisema asilimia 90 ya watendaji wa serikali katika wilaya hiyo wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakutoa huduma kwa wananchi, huku akiionyooshea kidole taasisi hiyo kwa kuwafumbia macho watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rombo.  "Nasikitika kusema kuwa asilimia 90 ya watendaji wa halmashauri wanafanya kazi kwa kupokea rushwa ili kuwaudumia wananchi. Niwaonye na niwaambie taarifa hizo tunazo na majina yenu tunayo. Jirekebisheni mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.  “Takukuru sidhani kama mnatambua wajibu wenu au nimeona jengo tu ambalo halina utendaji? Wananchi wengi wanashindwa kup...

Makala: Achana na Wasafi Festival; Diamond, Alikiba hadi Studio

Huwenda nyakati zikawalazimu Diamond Platnumz na Alikiba kuwa kitu kimoja kwenye muziki kwa sasa. Ni kipindi kirefu wameripotiwa kutoelewa ingawa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hilo.  Kwa sasa Diamond yupo katika pilika pilika za kuhakikisha tamasha lake la Wasafi Festival linafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wakati akieleza kuhusu ujio wa Wasafi Festival alieleza kuwa angetamani na Alikiba angekuwepo kitu ambacho kiliibua mjadala mpana zaidi.  Alikiba tayari amekubaliwa kuwa sehemu ya udhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Wengi wamesema huu ni mwanzo nzuri kwa wasanii hawa kurudisha ushirikiano wao na kufanya vitu vikubwa zaidi.  Kwanini Studio    Hapo jana Diamond Platnumz akiwahojiwa na kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya alisema si Alikiba kushiriki Wasafi Festival tu bali hata kufanya wimbo pamoja yupo tayari.  "sio tu Alikiba mtu yeyote ambaye anahisi kuna sehemu nikimuweka Diamond itanisaidia katika k...