Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Prof: JOYCE NDALICHAKO AMESEMA AFRICA ITAENDELEZWA NA WAAFRICA WENYEWE

mteulethebest Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa Maendeleo ni  kusaidia kukua kwa Maendeleo hayo. Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa  Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika nyanja za Kijamii na Kiuchumi  kwa lengo la kutimiza malengo ya bara hilo. “ Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia   vijana ambao wameandaliwa  vyema na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila kuhofia changamoto watakazokutana nazo,” alisisitiza Waziri Ndalichako Kiongozi huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kija...

Chadema watoa taarifa kuhusu Jeshi la Polisi kumshikilia dereva wa Mbowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelalamikia hatua ya  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumshikilia kwa siku mbili  mtumishi wao Williard Urassa.  Urassa ambaye ni dereva wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Taarifa iliyotolewa leo, Novemba 24, 2018 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imeeleza tangu Urassa alipokamatwa na polisi, jeshi hilo limekataa kumpatia dhamana huku likizuia mtu yeyote kuonana naye.  Hii ndio Taarifa kamili:   Kwa siku ya pili leo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Ndugu Williard Urassa, ambaye ni mtumishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Makao Makuu, bila kueleza sababu za kumshikilia, huku pia akinyimwa haki zake za msingi, kinyume cha sheria za nchi.  Ndugu Urassa ambaye ni Dereva wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama y...

Klabu bingwa Africa: Kinnah Phiri kuwinda Simba

Mbabane Swallows wamkabidhi Kinnah Phiri  mtihani wa Simba Kocha wa zamani wa Mbeya City, Kinnah Phiri amekabidhiwa jukumu la kuiongoza klabu ya Mbabane Swallows katika mechi dhidi ya Simba. Phiri amepewa jukumu hilo la muda mfupi kutokana na kocha mkuu wa Mbabane Swallows, Thabo Vilakati kutumikia adhabu ya kifungo cha mechi nne kutoka CAF kwa kosa la kumpiga muokota mpira. Simba itapambana na Mbabane Swallows katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumatano.

Hizi ndiyo njia za kulinda mafanikio yako

Maeneo nane unayotakiwa kuyatawala kiuhakika ili ufanikiwe Ushindi wowote katika mafanikio unapatikana kwa kutawala. Kwa mfano, Ili uweze kufanikiwa katika biashara unatakiwa kuitawala biashara hiyo katika kila eneo, kwa kuijua biashara hiyo ndani nje tena kwa uhakika.  Hata katika mafanikio kwa ujumla vipo vitu ambavyo unatakiwa kuvitawala, kwa jinsi unavyovitawala vitu hivyo unapata uhakika wa mafanikio kwa asilimia kubwa sana. Je, ni mambo yapi ambayo unatakiwa kuyatawala ili kufanikiwa?  1.  Jitawale wewe kwanza.   Kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukitawala vizuri ili ujijengee mafanikio ni kujua jinsi ya kujitawala wewe. Tambua jinsi ya kutawala fikra zako, matendo yako, vitu unavyosoma au kuangalia, imani na mitazamo uliyonayo juu ya maisha ya mafanikio.  Kwa kujua jinsi ya kutawala hayo mambo inakusaidia sana wewe kuweza kufanikiwa na kupiga hatua. Watu wanaofanikiwa wanajua sana jinsi ya kujitawala wao wenyewe hasa kutokana na kumudu kutawala ...

Watanzania washauriwa kukopa

Dkt. Mwakyembe : Woga wa kukopa ni tatizo kubwa kwa Watanzania Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema Watanzania waache kuogopa kukopa lakini benki nazo zibadilike.  Dkt. Mwakyembe amesema, woga wa kukopa ni tatizo kubwa kwa Watanzania na ni la kihistoria kwa kuwa zamani kuliko na sheria iliyowazuia wazawa wasikope kwa sababu iliwatambua kuwa ni watoto.  Waziri Mwakyembe amewaeleza wajumbe wa Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoa wa Tabora hali sasa imebadilika hivyo wananchi wakope wawekeze.  Tabora inabidi ibadilike hasa, isiwe Tabora ile ya maembe tunagawana na wadudu” amesema na pia amewaeleza viongozi kuwa uongozi si umasikini.  Dkt. Mwakyembe amesema, viongozi hawazuiwi kuwa matajiri ila watapaswa kueleza wameupata vipi utajiri huo na ndiyo maana kuna suala la maadili kwa viongozi wa umma.  Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Fursa za Biashara Tabora lililofanyika kwa siku tatu mjini Tabora. Waz...

Ndege mpya itakayonunuliwa na Tanzania ni ndege ya aina gani?

Airbus A220-300 Ndege mpya ambayo itakuwa ya karibuni zaidi kununuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege la Air Tanzania inakaribia kukamilika kutengenezwa. Ndege hiyo, ambayo inaundwa na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Airbus, itakuwa ya muundo wa A220-300. Ndege hiyo itakuwa na jina la Dodoma, mji mkuu rasmi wa Tanzania. Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa kuhamishia shughuli zake zote jijini Dodoma. ADVERTISEMENT Tanzania iliponunua ndege ya majuzi zaidi, 787-8 Dreamliner ya kampuni ya Boeing, ndege hiyo ilipewa jina la Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika. Sawa na ndege hiyo ya Dreamliner, ndege hiyo mpya ya Airbus ina nembo ya 'Hapa Kazi Tu' chini ya jina Dodoma. Hapa Kazi Tu imekuwa kauli mbiu ya Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli tangu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015. Kampuni ya Airbus Alhamisi iliandika ujumbe kwenye Twitter: "Kiwango cha joto ni chini ya sifuri hapa Mirabel, Canada lakini tw...

Alikiba sasa mimi ni baba kijacho

Alikiba akiri mkewe Amina ni mjamzito Kwa mara ya kwanza Staa wa Bongofleva  Alikiba amefunguka kuhusu Mke wake Amina kuwa na ujauzito katika mahojiano aliyoyafanya na Radio Jambo ya nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya kutangaza kinywaji chake cha MOFAYA nchini humo.  Alikiba amefunguka na kusema hakukutana na Mke wake Amina Mjini Mombasa kama Watu wanavyofikiri bali walikutana Nairobi na alikuwa kama Shabiki yake mkubwa na kipindi hicho Mke wake alikuwa akisoma katika Chuo cha United States International (USIU).  Baada ya Alikiba kuulizwa kuhusu Mke wake kama ni mjamzito alijibu hivi  >>>“Katika dini yetu tunaamini kwamba ni faida kubwa ya ndoa Mtu kupata ujauzito, kwa hiyo baada ya ndoa tu Mke wangu akapata baraka na Mungu akipenda mwakani tutabahatika kupata Mtoto, hatutajua ni Mtoto wa jinsia gani tunasubiria surprise na huyu atakayekuja atakua Mtoto wangu wa nne”