Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Chemical:- Natafuta mwanaume" -

Msanii wa kike wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chemical, ametangaza kutafuta mwanaume ambaye atakuwa mkweli ili awe naye kwenye mahusiano kwa malengo ya kufunga naye ndoa. Chemical amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo atatokea mwanaume ambaye atakuwa 'serious', hatosita kuwa naye. Kabla ya kufikia uamuzi huo Chemical alielezea juu ya kitendo cha kumtosa Stereo, na kusema kwamba msanii huyo alikuwa anamjaribu lakini aligundua hakuwa mkweli kwake, ndio maana ameamua kutafuta mtu ambaye atakuwa 'serious' naye. 'Wanaume wengi wanaumiza, kuna watu wanahisi Chemical haingii kwenye mahusiano, mimi ni mdada jamani naingia kwenye mahusiano, moyo wangu uko very delicate hivyo sipendi kuumizwa moyo, lakini akitokea mwanaume wa ukweli ambaye hatamuumiza Chemical, niko tayari kupenda na kupendwa, Stereo alikuwa anataka kunichezea, sijui alikuwa anataka kujaribu, hakuwa serious, mimi nilijifanya kumkataa kidogo tu akapat...

Tanzia: sita wafariki kwa ajali Morogoro

Watu sita wamefariki dunia kwa kwa ajali ya gari mkoani Morogoro, ambapo miongoni mwa waliofariki ni msanii maarufu wa muziki wa mchiriku na singeli kutoka kundi la 'Jagwa', Jack Simela. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro, baada ya gari lao dogo lililokuwa likitokea kwenye mazishi mkoani humo kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo, amethibitisha kupokea miili sita na majeruhi wawili, na kusema kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri hospitalini hapo. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijawekwa wazi, baada ya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro kugong mwamba. Jack Simela alikuwa ni muimbaji kiongozi wa kundi la Jagwa Music ambalo ni maarufu kwa muziki aina ya mchiriku, muziki ambao umekuwa ukipendwa na mataifa ya nje ikiwemo Ujerumani, ambako ndiko mara nyingi yeye na kundi lake walikuwa wakienda kufanya matamasha.         ...

River Plate Bingwa wa Copa Libertadores

River Plate Bingwa wa Copa Libertadores , ilikuwa game ya kihistoria Bernabeu Fainali ya Kombe la  Copa Libertadores  kati ya River Plate  na  Boca Junior  unaweza kuiita fainali ya kusisimua katika soka usiku wa December 9 2018, mvuto wa fainali hiyo unakuja kutokana na kuzikutanisha timu wapinzani ambao wamesabisha kiasi cha game hiyo kushindwa kuchezwa  Argentina  na kupelekwa katika jiji la  Madrid  katika uwanja wa  Santiago Bernabeu. Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mastaa kibao wa soka akiwemo  Lionel Messi  wa  FC Barcelona  na  Antoine Griezmann  wa  Atletico Madrid , ulimalizika kwa  River Plate  kupata ushindi wa magoli 3-1, hiyo wanashinda taji hilo kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-3, kwani mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2. Ubingwa wa  Copa Libertadores   kwa  River Plate  unakuwa ni Ubingwa wao wa nne katika histori...

Vyama 15 vya upinzani vyaungana

Vyama vya upinzani 15 nchini vimeungana kupinga muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ambao ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni mwezi uliopita wakati wa mkutano wa 13 wa Bunge. Baadhi ya viongozi wa vyama vilivyoshiriki kutoa tamko la pamoja Vyama vilivyoshiriki katika kutoa tamko la pamoja kupinga muswada huo ni CHADEMA, CUF, DP, ACT Wazalendo, NLD, ADC, CCK, UPDP, Chauma, NCCR Mageuzi vikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chauma), Hashim Rungwe. Akisoma tamko la pamoja katika mkutano huo, Mwenyekiti wa muungano huo, Hashim Rungwe amesema kuwa wameamua kuichagua siku ya leo ya Uhuru kwakuwa ni siku muhimu ya kukumbukwa kwa nchi japokuwa haijasheherekewa kama ilivyozoeleka. " Tumeitumia siku ya leo ya Uhuru kutoa tamko hili kwani ni siku muhimu kwa taifa letu na serikali ya awamu ya tano kuendelea kufuta sherehe za Uhuru ambazo Duniani kote ni siku ambayo taifa husheherekea kuzaliwa kwake , " amesema. Kuhusu msimamo wa umoja huo kwenye sheria ...

Waafrika Kusini waandamana kisa Makonda

Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania, wakipinga kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa wake. Wananchi hao ambao idadi yao haikujulikana kwa mara moja, pia wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini. “ Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu, tunakutaka uwape hifadhi watu hawa  wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu ”, walisikika waandamani hao kwenye ujumbe wao. Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na...

Mfungwa achagua kuuawa kwa kutumika kiti cha umeme badala ya sindano ya sumu Marekani

The electric chair has gradually been replaced as the main method of execution Mfungwa mmoja katika jimbo la Tennessee nchini Marekani atauawa kwa kiti cha umeme baada ya kudai kuwa sindano ya sumu itasababisha ateseke. David Earl Miller, ambaye amekuwa kwenye hukumu ya kifo kwa miaka 36 ni kati ya wafungwa wanaoongezeka wanaojaribu kukwepa sindano ya sumu kufuatia visa kadhaa vya kufeli. Mfungwa mwingine huko Tennessee Edmund Zagorski, aliuawa kwa njia ya umeme mwezi uliopita. Kuuliwa kwa kutumia sindano ya sumu ndiyo njia kuu ya kuwaua wafungwa katika jimbo hilo. Hata hivyo wafungwa katika jimbo hilo ambao walitenda uhalifu kabla ya mwaka 1999 wataruhusiwa kuchagua kuuliwa kwa njia ya umeme. Mahakamani, Miller na Zagorski walitaja kisa cha kuuuliwa Billy Ray Irick cha mwezi Agosti ambaye alibadilika rangi kuwa Zambarau na kuchukua dakika 20 kufa. Kuuliwa kwa Zagorski ilikuwa mara ya pili kiti cha umeme kimetumiwa katika jimbo hilo tangu mwaka 1960. Miller alikutwa na ha...

Magufuli amgusia Lowassa kuhusu maji

Rais Dkt. John Magufuli amezungumzia kitendo cha Mbunge wa Monduli (CCM), Julius Kalanga kumuomba apeleke maji jimboni kwake ilihali jimbo hilo limewahi kuongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye pia amewahi kuwa waziri wa maji. Rais Dkt. Magufuli akiwa na Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Akizungumza na wananchi wa Arumeru, ambapo amezindua na kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 jijini Arusha, Rais Magufuli amesema kuwa anampongeza Kalanga kwa kuhamia CCM akitokea CHADEMA kwakile alichosema ni kitendo cha kijasiri. " Kalanga,  Mbunge wa Monduli aliwahi kuniomba maji akiwa CHADEMA, lakini amesahau kuwa Lowassa amewahi kuwa Waziri wa Maji, simsemi mzee wangu namaanisha kuwa uzalendo unaanzia nyumbani, nikupongeze Kalanga kwa ujasiri wako wa kurudi huku, maji utapata ", amesema Rais Magufuli Katika hatua nyingine amewaomba Watanzania kumuombea ili awatumikie vyema, " Muendelee kuniombea ili cheo changu cha Urai...