Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine

Seneta Rand Paul katikati akiwa na marafikize kutoka kwa bunge la uwakilishi muda mfupi baada ya bunge la seneti kuitisha mapumziko Huduma za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa. Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika. Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi. Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu. Hatahivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini. Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili. Maboksi ya pizza yalipelekwa katika bunge hilo huku watu wakita...

Dadake kiongozi wa Korea Kaskazini kutembelea K Kusini kwa ajili ya michezo ya Olimpiki

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwanamke aliye na ushawishi mkubwa Korea Kaskazini atahudhuria michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itakayozinduliwa Pyeongchang ,siku ya Ijumaa, mawaziri jijini Seoul wanasema. Kim Yo-jong, atakuwa ndugu wa kwanza wa karibu katika familia ya Kim atakayevuka mpaka. Korea zote mbili zitaandamana pamoja chini ya bendera moja katika sherehe za uzinduzi. Ushiriki wa Korea Kaskazini umeonekana kama kulegeza uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Hata hivyo, Marekani na Japan wameishtumu Korea Kaskazini kwa kutumia michezo hio kama chama cha propaganda. Kim Yo-jong  ni nani ? Akiaminiwa kuzaliwa mwaka 1987, ni mtoto wa kike wa mwisho wa hayati kiongozi Kim Jong-il na ni dada yake wa tumbo moja Kim Jong-un. Anazidiwa umri na kaka yake kwa miaka minne na inasemekana kwamba wana uhusiano wa karibu sana. Anasemekana kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala. Kim Yo-jong akiwa kwenye sherehe ya kuzindua jengo la ...

Kenya yatetea uamuzi wa kumfukuza Miguna

Bwana Miguna Miguna na Raila Odinga Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake Jana usiku mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana Miguna Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009. "Kwa mantiki hiyo hati ya kusafiria ya Kenya ya bwana Miguna ilikuwa na bado ni batili", alifafanua bwana Njoka Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baad...

mamia waandamana nje ya ubalozi wa Rwanda,Israel

Waandana nje ya ubalozi wa Rwanda Mamia ya waandamanaji wamekusanyika nje ya ubalozi wa Rwanda nchini Israel katika mji wa Herzeliya kulalamikia sheria mpya ya wahamiaji nchini humo. Wengine wakiwa wamebeba mabango yanayosema "nitafukuzwa mpaka nife kwa sababu mimi ni mweusi"kutokana na mapendekezo ya kuwa wahamiaji kutoka Afrika hawakaribishwi nchini Israel kuliko wahamiaji kutoka bara la ulaya kwa sababu ya ubaguzi wa rangi. Waandamanaji wa Afrika nchini Israel Wahamiaji wengi wa Afrika nchini Israel wanatoka Eritrea na Sudan Kusini Maandamano hayo nje ya ubalozi wa Rwanda yalikuwa yanamtaka Rais Paul Kagame ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na rais wa Rwanda kupinga mpango wa Israel wa kuwaondoa wahamiaji 38,000 ambao wengi wao ni kutoka Eritrea na wenye asili ya Sudan Kusini. Mwanzoni mwa mwaka ,serikali ya Israel ilitoa taarifa kwa maelfu ya wahamiaji wa Afrika kuondoka nchini humo au watakabiliana na kifungo. Inasemwa kuwa wahamiaji...

Miguna Miguna kutoka Kenya

Serikali yamfurusha Miguna Miguna na kumpeleka Canada Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefurushwa na kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM , kulingana na wakili wake Nelson Havi na Cliff Ombeta. Bwana Ombeta amesema kuwa aliarifiwa kwamba bwana Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada. Wakili mwengine Dkt. John Khaminwa alisema kuwa mteja wake tayari ameondoka Kenya. "Ni kweli .Alilazimishwa kuingia katika ndege ya KLM dakika chache tu kabla ya saa nne usiku na tumebaini kwamba anaelekea Canada. Ni ukiukaji mkubwa wa haki'', alisema Dkt Khaminwa kwa simu. Haijulikani ni sheria gani iliotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo. Anasema kwamba wakati Miguna alipokamatwa , serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia Kenya kionyesha wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na wali...

Esmond Bradley Martin: Mchunguzi jasiri aliyewakabili wawindaji haramu AUAWA Nairobi

Esmond Bradley Martin amejitolea maisha yake kupiga picha na kukusanya taarifa kuhusu biashara ya uwindaji haramu wa pembe za tembo na vifaru Esmond Bradley Martin, mojawapo ya wachunguzi wakuu duniani dhidi ya biashara haramu ya kimataifa ya pembe za tembo na vifaru, amepatikana amedungwa kisu na kuuawa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi. Alifanya uchunguzi wa siri katika baadhi ya maeneo hatari na magumu duniani, akipiga picha na kuorodhesha masoko ya pembe hizo, akizungumza na walanguzi, na kufanya hesabu za bei katika soko haramu la biashara hiyo yote katika jitihada za kuwaongoza waundaji sera katika uhifadhi wa mzingira. Katika miaka kadhaa ya nyuma, alisafiri kwenda China, Vietnam na Laos na mratibu Lucy Vigne, wakifika katika maeneo ambayo watu wachache wa mataifa ya nje wangesubutu kuyakanyaga, wakijifanya kuwa wanunuzi wa pembe za tembo na vifaru. Katika eneo la kucheza kamari linalomilikiwa na Wachina huko Laos, wapenzi hawa wasio wa kawaida walipishana na majang...

Dada yake mwimbaji maarufu Mowzey Radio aliyefariki wiki iliyopita amekamatwa kama mtuhumiwa katika kesi ya kaka yake

Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe Polisi nchini Uganda wamemkamata mtuhumiwa anayehusishwa na mauaji ya mwanamuziki maarufu Mowzey Radio, aliyefariki kutokana majeraha aliyoyapata baada ya mzozo uliotokea kwenye kilabu moja ya usiku '' De Bar'', iliyopo katika mji wa Entebbe. Wakati wa mazishi yake, mama yake Jane Kasumba aliwalaani wauaji wake imeripotiwa katika magazeti ya Daily Monitor. Amenukuliwa akisema: Nimeumizwa sana, sana. Lakini kinachoniumiza zaidi ni kwamba sikuwaona waliomuua mwanangu. Ninawalaani waliomuua mwana wangu. " "Utawala wa hospitali ya Case wanasikitika kutangaza kifo cha Moses Ssekibogo maarufu kama Mowzey Radio leo tarehe 1 Februari 2018 saa kumi na mbili asubuhi," ilisoma sehemu ya taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Case kuhusiana na kifo chake. Radio, ambaye jina lake halisi Moses Ssekibogo, alifariki kutokana na majeraha yaliyoto...