Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

UTAJIRI WA PUTIN HUU HAPA

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin. RAIS wa Urusi, Vladimir Putin akiwa amebakiza siku chache kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu, ameanika kiasi cha fedha alizojipatia kipindi cha miaka mitano iliyopita ambacho si kikubwa kama ambavyo ilifikiriwa.   Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Urusi imeeleza kuwa, Rais Putin alijipatia mapato ya Rouble Milioni 38.5 za Urusi sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 1.9 kati ya mwaka 2011 na 2016. Hiyo maana yake ni kwamba kiongozi huyo wa nchi ya Urusi ana mshahara wa Dola za Kimarekani 143,000 kwa mwaka.   Fedha hizo hazizidi hata theluthi moja ya ule anaopokea Waziri Mkuu wa Australia, Malcom Turnbull ambaye hulipwa Dola za Kimarekani 527,852. Kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post, Rais Putin pia ameorodhesha akaunti 13 za benki mbalimbali ambazo kwa pamoja zina akiba ya Dola za Kimarekani 307,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 650.   Rais Putin pia ameorodhesha kumiliki nyumba zake mjini St Petersburg, ...

Trump lawamani na sheria ya silaha

Shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouwawa Chama cha Democrats kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha. Hii imetokea siku moja baada ya wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani. Wakati huo huo shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouawa kwenye tukio hilo imefanyika huko Florida kulikotokea tukio hilo. Wakati wa Marekani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza kifo cha wanafunzi 17 waliuawa kwa kupigwa risasi kumekuwa na wito wa nchi hiyo kubadili sheria ya kumiliki silaha. Rais Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari baada ya shambulio Akizungumzia mauaji hayo Rais wa Marekani Donald Trump awali katika hotuba yake amesema usalama katika shule utakuwa ni moja ya mambo yatakayopewa kipau mbele. Hata hivyo alishindwa kulishauri bunge la nchi hiyo lipitie upya sheria ya kumiliki silaha. "Utawala wetu unafanya kazi kwa karibu na ma...

Watanzania wawili kunyongwa China, mtoto arudishwa

Watanzania wawili mume na mke waliotambulika kwa majina ya Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa wamekamatwa na dawa za kulevya China katika uwanja wa ndege wa   Baiyun Guangzhou wakiwa na mtoto wao mdogo wa miaka 2 ambaye amerudishwa leo nchini Tanzania Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Sheria za Madawa ya kulevya , Edwin Kakolaki amesema kuwa raia hao wa Tanzania Januari 19, 2018 uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya , walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda , Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82. Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini , mtoto huyo amewasili leo nchini Tanzania na Serikali kusema kuwa watafanya utaratibu wa kuhakikisha wanawatafuta ndugu wa watu hao ili waweze kuwakabidhi mtoto huyo ....

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine

Seneta Rand Paul katikati akiwa na marafikize kutoka kwa bunge la uwakilishi muda mfupi baada ya bunge la seneti kuitisha mapumziko Huduma za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa. Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika. Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi. Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu. Hatahivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini. Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili. Maboksi ya pizza yalipelekwa katika bunge hilo huku watu wakita...

Dadake kiongozi wa Korea Kaskazini kutembelea K Kusini kwa ajili ya michezo ya Olimpiki

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwanamke aliye na ushawishi mkubwa Korea Kaskazini atahudhuria michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itakayozinduliwa Pyeongchang ,siku ya Ijumaa, mawaziri jijini Seoul wanasema. Kim Yo-jong, atakuwa ndugu wa kwanza wa karibu katika familia ya Kim atakayevuka mpaka. Korea zote mbili zitaandamana pamoja chini ya bendera moja katika sherehe za uzinduzi. Ushiriki wa Korea Kaskazini umeonekana kama kulegeza uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Hata hivyo, Marekani na Japan wameishtumu Korea Kaskazini kwa kutumia michezo hio kama chama cha propaganda. Kim Yo-jong  ni nani ? Akiaminiwa kuzaliwa mwaka 1987, ni mtoto wa kike wa mwisho wa hayati kiongozi Kim Jong-il na ni dada yake wa tumbo moja Kim Jong-un. Anazidiwa umri na kaka yake kwa miaka minne na inasemekana kwamba wana uhusiano wa karibu sana. Anasemekana kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala. Kim Yo-jong akiwa kwenye sherehe ya kuzindua jengo la ...

Kenya yatetea uamuzi wa kumfukuza Miguna

Bwana Miguna Miguna na Raila Odinga Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake Jana usiku mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana Miguna Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009. "Kwa mantiki hiyo hati ya kusafiria ya Kenya ya bwana Miguna ilikuwa na bado ni batili", alifafanua bwana Njoka Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baad...

mamia waandamana nje ya ubalozi wa Rwanda,Israel

Waandana nje ya ubalozi wa Rwanda Mamia ya waandamanaji wamekusanyika nje ya ubalozi wa Rwanda nchini Israel katika mji wa Herzeliya kulalamikia sheria mpya ya wahamiaji nchini humo. Wengine wakiwa wamebeba mabango yanayosema "nitafukuzwa mpaka nife kwa sababu mimi ni mweusi"kutokana na mapendekezo ya kuwa wahamiaji kutoka Afrika hawakaribishwi nchini Israel kuliko wahamiaji kutoka bara la ulaya kwa sababu ya ubaguzi wa rangi. Waandamanaji wa Afrika nchini Israel Wahamiaji wengi wa Afrika nchini Israel wanatoka Eritrea na Sudan Kusini Maandamano hayo nje ya ubalozi wa Rwanda yalikuwa yanamtaka Rais Paul Kagame ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na rais wa Rwanda kupinga mpango wa Israel wa kuwaondoa wahamiaji 38,000 ambao wengi wao ni kutoka Eritrea na wenye asili ya Sudan Kusini. Mwanzoni mwa mwaka ,serikali ya Israel ilitoa taarifa kwa maelfu ya wahamiaji wa Afrika kuondoka nchini humo au watakabiliana na kifungo. Inasemwa kuwa wahamiaji...