Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mwanamfalme wa Saudia asema hana mpango wa kuinunua klabu Manchester United:

Manchester United: Mwanamfalme wa Saudia asema hana mpango wa kuinunua klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amekanusha madai kuwa anantaka kuinunua Manchester United kwa kitita cha pauni bilioni 3.8. Tetesi ziliibuka mwishoni mwa wiki zikimuhusisha mwanamfalme huyo na kutaka kuinunua klabu hiyo tajiri nchini Uingereza. Wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazers wanadaiwa kuwa hawana mpango wa kuiuza timu yao. Wamiliki hao kutoka Marekani waliinunua Man United kwa kitita cha pauni milioni 790 mwezi Mei 2005. "Ripoti zinazomuhusisha Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman kuwa anataka kuinunua Manchester United ni uongo mtupu," amesema waziri wa michezo wa Saudia Turki al-Shabanah. "Manchester United walifanya mkutano na mfuko wa uwekezaji wa umma PIF wa Saudia kuhusu nafasi ya udhamini. Lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa," ameeleza waziri huyo. Salman, 33, aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha ...

KUTANA NA TIMU IYOFUNGWA GOLI 20 JUMAPILI HII

Klabu ya Pro Piacenza yalazwa 20-0 katika mechi ya ligi Serie C Iwapo unadhania timu yako imekuwa na msururu wa matokeo mabaya wikendi hii basi fikiria kichapo hiki walichopewa Pro Piacenza katika ligi ya Itali. Klabu hiyo ya ligi ya Serie C iliowekwa katika kundi A ilishindwa magoli 20-0, ' ndio magoli ishirini bila jibu ' na wapinzani wao katika ligi hiyo Cuneo siku ya Jumapili jioni. Walikuwa nyuma kwa magoli 16 kwa bila wakati wa muda wa mapumziko huku mshambuliaji wa Cuneo Hicham Kanis akifunga magoli sita pekee kabla ya mapumziko naye mshambuliaji mwenza Eduardo Defendi akipata magili matano. Katika safu ya ulinzi ya Pro Piacenza kulikuwa na matatizo yaliosababisha mvua hiyo ya magoli. Wakiwa chini katika ligi hiyo ya tatu ya Itali, klabu hiyo ya kaskazini ina matatizo makubwa ya ufadhili. Walipokonywa pointi nane mapema katika kampeni yao na wameripotiwa kushindwa kuwalipa wachezaji wao tangu mwezi Agosti hatua iliosababisha kujiuzulu kwa wachezaji wengi wa ki...

Rais Vladimir Putin amesema Urusi itaanza kuunda makombora mapya

  Marekani inahofia makombora mapyaya Urusi Urusi imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi sawa na huo uliyochukuliwa na Marekani. Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo litaanza kuunda makombora mapya. Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake siku ya Ijumaa. Mkataba huo uliyofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Sovieti, USSR na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri. "Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,"alisema Bw. Putin siku ya Jumamosi. Urusi ilirusha kombora katika mazoezi ya kijeshi Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya magharibi Nato, Jens Stoltenberg amaiambia kuwa: "Washirika wote [Ulaya] yameunga mkono hatua ya Marekani kwasababu Ur...

Ole Gunnar Solskjaer kupewa kazi Manchester United akishinda Paris St-Germain

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 02.02.2019: Solskjaer, Hudson-Odoi, Willian, Bakayoko Manchester United hawajashindwa hata mechi moja chini ya uongozi wa Ole Gunnar Solskjaer Manchester United watampatia kazi meneja wao wa sasa Ole Gunnar Solskjaer akifanikiwa kushinda Paris St-Germain katika mchuano wao wa ligi ya mabingwa. (Sun) Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ameelezea kutoridhishwa kwake na usimamizi wa klabu hiyo baada ya kushindwa kusajili wachezaji wapya kwa misimu miwili mfululizo. (Mirror) Chelsea watakabiliana na Bayern Munich katika uhamisho wa mshambuliaji Callum Hudson-Odoi, baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kushindwa kumsajili nyota huyo wa miaka. (Sun) Hudson-Odoi, wa kati Winga Willian, 30 wa Chelsea na Brazil, anataka kusaini mkataba wa miaka mitatu, lakini kuna tetesi amepewa mkataba wa mwaka mmoja. (Sport Witness) Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini alitaka kumsaini mchezaji wa zamani wa Cardiff, Gary Medel mwezi Januari lakini juhudi zake zili...

Rajoelina atangazwa mshindi uchaguzi wa Madagascar

Kiongozi wa zamani wa Madagascar Andry Rajoelina ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa taifa hilo la kisiwa cha bahari ya Hindi katika matokeo ya awali yaliotangazwa na tume ya uchaguzi Alhamisi. Rajoelina alikuwepo wakati tume ya uchaguzi ikitangaza kwamba amepata asilimia 55.66 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 44.34 ya mshindani wake Marc Ravalomanana - ambaye hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo. Ravalomanana, ambaye pia ni rais wa zamani, amekosoa uchaguzi katika kisiwa hicho kilichoko nje ya pwani ya Afrika kwa kile alichokiita udanganyifu mkubwa. Mahakama ya katiba hivi sasa ina muda wa siku tisa kutangaza matokeo ya mwisho. Siasa nchini Madagascar, ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa na mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, kwa muda mrefu zimekuwa zikizongwa na mapinduzi ya mara kwa mara na machafuko. Rajoelina na Ravalomamana wana historia ya uhusiano mgumu kati yao, baada ya Rajoelina kuchukuwa nafasi ya Ravalomana kama akiongozi wa taifa kufuati...

Aanza safari ya kuvuka bahari ya Atlantiki kwa kutumia pipa

Jean-Jacques Savin: Raia wa Ufaransa Jean-Jacques Savin ametumia miezi kadhaa kutengeneza pipa hilo katika chelezo kimoja kusini magharibi mwa Ufaransa Bwana mmoja raia wa Ufaransa ameanza safari ya kuvuka bahari ya pili kwa ukubwa duniani, Atlantiki, kwa kutumia pipa kubwa aliloliunda mwenyewe. Jean-Jacques Savin, mwenye miaka 71, ameanzia safari hiyo kutoka mji wa El Hierro uliopo kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania na anataraji kufika visiwa vya Caribbean ndani ya miezi mitatu. Pipa hilo linategemea nguvu ya msukumo ya mawimbi pekee kufanikisha safari. Ndani ya pipa hilo kuna sehemu ya kulala, jiko na stoo ya kuhifadhi vitu. Bwana Savin pia atakuwa anaweka alama katika safari yake ili kuwawezesha wataalamu wa bahari kuyafanyia tafiti zaid mawimbi ya bahari ya Atlantiki. Taarifa zote kuhusu mwenendo wa safari hiyo zinawekwa kwenye  ukurasa maalumu wa mtandao wa Facebook  na ujumbe wa mwisho umeeleza kuwa pipa lilikuwa linaenda vizuri. Katika mahojiano kwa...

TCAA yafafanua kuhusu kuzuia ndege za Masha

Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA nchini imekanusha taarifa ya kuzuiwa kwa ndege za Shirika la Ndege la Fastjet, kama ilivyoelezwa na Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo Laurence Masha, kwa kile ilichokisema ilipokea barua ya shirika hilo Desemba 24 mwaka huu. Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la FastjetLawrence Masha. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema baadhi ya barua za kuomba kuwasilisha ndege hizo zilifikishwa kwao Desemba 24 na hazikushughulikiwa kutokana na kuwa ni kipindi cha sikukuu. " Nakanusha taarifa si za kweli hatujawahi kukataa ombi la kuleta ndege na hatuwezi kukataa kwa sababu ni maagizo tuliyowaambia ." amesema Johari. " Walileta andiko la mabadiliko ya utawala na fedha tarehe 24 Desemba mwaka huu , na wataalamu wameanza kulifanyia kazi na muda si mrefu tutawajibu ," ameongeza. Aidha Mkurugenzi huyo amesema miongoni mwa masharti am...