Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 17.11.2019:

Gareth Bale Manchester United wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale,30, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Sun on Sunday) Paris St-Germain wanawezekana kuwa kikwazo kikubwa kwa mpango wa Manchester United wa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19 mwenye thamani ya pauni milioni 120. (Sunday Express) PSG pia wanamtaka kiungo wa Liverpool Adam Lallana,31.(Sunday Mirror) Manchester United wanamtazama kwa karibu winga wa West Bromwich Albion Matheus Preira, anayecheza kwa mkopo akitokea Sporting Lisbon. (Mirror) Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho Arsenal wanajiandaa kumuwania mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uturuki, ambaye anaweza kuuzwa na Juventus kama ofa ya kuridhisha itatolewa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.(Tuttosport - in Italian) Barcelona wanajadili mkataba mpya na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32. (Mundo Deportivo - in Spanish) Mshambuli...

Maandamano ya kumuunga mkono Morales

Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika ubalozi wa Bolivia nchini Argentina wakimuunga mkono Evo Morales Mamia ya watu nchini  Argentina  wameandamana kuonyesha kumuunga mkono  Evo Morales   Rais wa  Bolivia  aliyelazimisha na jeshi la nchi hiyo kujiuzulu. Raia wa Bolivia wanaoishi nchini Argentina kwa uratibu wa asasi za kiraia zenye mrengo wa kushoto walikusanyika mbele ya ubalozi wa Bolivia nchini Argentina. Waandamanaji hao walilaani hila alizofanyiwa Rais Morales katika uchaguzi na baada ya uchaguzi na kutolea wito jamii la kimataifa kumuunga mkono Morales. Waandamanaji hao walibeba mabongo yenye ujumbe kama “Hatutaki mapinduzi Bolivia” pia walikuwa wakipeperusha bendera yenye rangi 7 inayowakilisha wakazi wa  eneo la milima ya Andes pamoja na bendera za Bolivia.

Msuva, Sure boy , Samatta moto wao nimkali

Sure Boy aipa Taifa Stars kuvuna alama tatu katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon 2021 baada ya kuifunga Guinea ya Ikweta mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa ulishuhudiwa  Stars wakiutawala kwa asilimia kubwa lakini iliweza kujikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma bao 1-0. Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa wenyeji kuutawala kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na nahodha wa  Stars, Mbwana Samatta aliyekuwa akisaidiana na Simon Msuva kuliandama lango la wapinzani. Samatta alikosa kuiandikia bao Stars dakika ya pili baada ya mpira wake kuokolewa na Mlinda mlango wa Felipe Ovono ambaye alionesha umahiri wake wa kuokoa michomo. Wakati vijana hao wa Kocha, Etienne Ndayiragije wakiendelea kulisakata soka mbele ya watazamaji waliojitokeza kwa wingi kutoa sapoti, walijikuta wakiruhusu bao dakika ya 15 lililofungwa na Petro Obiang ambalo lilidumu hadi mapumziko. Hata hivyo Samatta alikosa nafasi nyingne ya kuisawazishia Stars dakika ya 40 l...

Msuva, Sure boy , Samatta moto wao nimkali

Sure Boy aipa Taifa Stars kuvuna alama tatu katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon 2021 baada ya kuifunga Guinea ya Ikweta mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa ulishuhudiwa  Stars wakiutawala kwa asilimia kubwa lakini iliweza kujikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma bao 1-0. Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa wenyeji kuutawala kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na nahodha wa  Stars, Mbwana Samatta aliyekuwa akisaidiana na Simon Msuva kuliandama lango la wapinzani. Samatta alikosa kuiandikia bao Stars dakika ya pili baada ya mpira wake kuokolewa na Mlinda mlango wa Felipe Ovono ambaye alionesha umahiri wake wa kuokoa michomo. Wakati vijana hao wa Kocha, Etienne Ndayiragije wakiendelea kulisakata soka mbele ya watazamaji waliojitokeza kwa wingi kutoa sapoti, walijikuta wakiruhusu bao dakika ya 15 lililofungwa na Petro Obiang ambalo lilidumu hadi mapumziko. Hata hivyo Samatta alikosa nafasi nyingne ya kuisawazishia Stars dakika ya 40 l...

Mashambulio ya angani yakwamisha amani Israel na Gaza

Gaza imeshuhudia mashambulizi zaidi ya angani baada ya roketi kuelekezwa Israel Israel imefanya mashambulio mapya ya angani dhidi ya ngome ya wanamgambo baada ya roketi iloyorushwa kutoka Gaza kuanguka katika eneo lake, hatua ambayo huenda ikalemaza juhudi za kusitisha mapigano. Vyombo vya habari vya Palestina vinasema makombora ya Israel yalilenga maeneo yanayokaliwa na kundi la Kipalestina la Islamic Jihad (PIJ) mapema siku ya Ijumaa, na kuwajeruhi. Hii ni baada ya roketi tano kurushwa katika ardhi ya Israel Alhamisi baada ya PIJ kuitikia wito wa kusitisha mapigano. Ushawishi wa Iran 'unaongezeka' mashariki ya kati Mapigano yalizuka baada ya Israel kumuua kamanda wa PIJ siku ya Jumatatu. Israel ilisema Baha Abu al-Ata alikuwa "mtu hatari"ambaye alihusika kupanga shambulio la roketi la hivi karibuni kutoka Gaza. Zaidi ya maroketi 450 yalirushwa Israel, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa kutoka Gaza katika muda wa siku mbili . Mzozo kati ya Isr...

Serikali kujenga mabweni wanafunzi wasipate mimba

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesema mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari, ili kuwanusuru na wanafunzi wa kike na suala la mimba. Mwanafunzi mwenye mimba Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 15, 2019 wakati wa kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa Wabunge kwenda kwa Mawaziri. Waitara amesema kuwa " mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari ili watoto wakike wapate sehemu za kukaa na tuwaepushe na mimba zitakazowafanya washindwe kuendelea na masomo ." Leo Novemba 15, 2019 Bunge hilo linatarajiwa kuahirishwa baada ya kujadili mpango wa maendeleo ya Taifa kwa mwaka ujao wa fedha. Serikali kujenga mabweni ili wanafunzi wasipate mimba.

Tanzania :- Marekani na Uingereza zatilia shaka 'haki za Binadamu kisheria'

Tamko la Marekani na Uingereza linagusia kesi ya Erick Kabendera kama mfano wa hivi karibuni Ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania." Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria. "Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo. "Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria k...