Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Fahamu mikoa inayoongoza kwa UKIMWI

MTEULE THE BEST Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Jana 20 Disemba 2017, alimkabidhi Rais John Pombe Magufuli   takwimu inayoonyesha  hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), wakati wa uwekaji wa jiwe  la msingi katika ofisi za Takwimu Mjini Dodoma. Dkt. Mpango alisema  kuwa  takwimu za utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa juu ya hali ya maambukizi ya VVU,  inaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe ndo unaoongoza kwa maambukizi  ya VVU, na utafiti huo uliwahusisha   watu wenye umri wa miaka 15-49 kwa mwaka 2016-17. "Kiwango cha maambukizi mapya bado kiko juu kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ikiongozwa na Njombe 11.6%, Iringa 11.2% na Mbeya 9.2%. Mikoa yenye maambukizi ya kiwango cha chini ni Unguja 0%, Kaskazini Pemba 0%, Lindi 0.3%, Manyara 1.8% na Arusha 1.9%.", amesema Dkt. Mpango. Mara baada ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo Rais Magufuli aliwatak...

Magufuli aunda tume kuchunguza mali za CCM

MTEULE THE BEST Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo Disemba 20, 2017 ameunda tume ya watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini katika wajumbe hao yupo Wakili Albert Msando Magufuli amesema hayo leo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kikao chake cha kwanza ambacho kimefanyika mjini Dodoma. Aidha Magufuli amewataka watu ambao wanashikilia mali za chama hicho wajitokeze na kutoa ushirikiano kwa watu hao huku akiwasisitiza wanachama wa CCM nao kutoa ushirikiano ili mali zao zisipotee. 

DCI azungumzia tukio la Lissu na Ben Sanane

MTEULE THE BEST Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), amefunguka na kusema wao wanaendelea na upelelezi juu ya taarifa ya kutekwa kwa Ben Saanane na kudai hawawezi kusema kila hatua wanayochukua pia amedai polisi wanachukulia 'serious' shambulio la Lissu DCI Boaz amesema hayo leo Disemba 20, 2017 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia.  "Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu imeshafanyika...

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 20.12.2017

MTEULE THE BEST Image caption Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kutoa rekodi ya dau la Uingereza la £90m kumnunua mchezaji wa Chelsea na Ubelgiji ,26, Eden Hazard. (Sun) Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kutoa rekodi ya dau la Uingereza la £90m kumnunua mchezaji wa Chelsea na Ubelgiji ,26, Eden Hazard. (Sun) Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright ameitaka klabu ya Manchester City kumnunua mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah. (Sky Sports via the Daily Express) Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce anataka kumpatia mshambuliaji wa Uingereza na Arsenal Theo Walcott, 28, njia ya kuondoka Arsenal mbali na kumyakua kiungo wa kati wa Sevilla na Ufaransa Steven N'Zonzi, 29. (Daily Mirror) Newcastle United imejiunga katika harakati za kumsajili beki wa Chelsea David Luiz katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , lakini inataka kumchukua mchezaji huyo wa Brazil kwa mkopo (Shields Gazette) Atletico Madrid wako tayari kumuuza mshambuliaji...

Je, rais Zuma atang'atuliwa madarakani kufuatia mabadiliko ya uongozi wa ANC?

MTEULE THE BEST Image caption Jacob Zuma amekuwa Rais wa ANC kwa miaka kumi sasa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma inawezekana asimalize muhula wake wa mwisho madarakani baada ya chama cha ANC kumchagua Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake mkuu. Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Ramaphosa alikua rafiki wa karibu wa Zuma na hata msaidizi wake, lakini uhusiano wao umekua wa mashaka siku za karibuni. Ramaphosa anasema atapambana na rushwa jambo ambalo kwa Zuma limekua kama mzigo. Hivi ni vitu vichache ambavyo vinaweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2019: 1.Zuma kutimuliwa Image caption Muhula wa Rais Zuma kuiongoza Afrika Kusini unaisha mwaka 2019 Chama cha ANC kitapendelea kuona kiongozi mkuu wa chama akiwa pia Rais wa nchi, jambo ambalo kama litatokea litamfanya Zuma kuachia ngazi ama kutimuliwa. Hii itafungua njia kwa Ramaphosa kuchukua madaraka na kujaribu kurudisha imani ya wengi iliyopotea juu ya chama hicho kinachotuhumiwa na ufisadi, huku asilimia...

Bunge la Seneti lapitisha mswada wa kupunguza kodi Marekani

MTEULE THE BEST Image caption Makamu wa Rais Mike Pence alitangaza matokeo ya kura hizo Bunge la Seneti la Marekani limepitisha mswada ambao ulidumu kwa kwa zaidi ya miongo mitatu. Bunge la wawakilishi lilipitisha mswada huo mapema leo.Republican wana idadi kubwa ya wabunge nchini Marekani, hiyo ikitajwa kuwa sababu mojawapo ya kupitishwa kwake licha ya awali kupingwa na baadhi ya wabunge wa chama tawala. Mswada huo sasa utarudishwa bungeni siku ya Jumatano kwa hatua za kuitambua na kuiidhinisha moja kwa moja. Iwapo itapita kama ilivyotarajiwa, itakuwa mafanikio makubwa sana kwa Rais Trump tokea aingie madarakani. Wakosoaji wanasema sheria hiyo itapendelea zaidi watu matajiri kuliko wale wa tabaka la kati ama la chini. Image caption Mswada huo unatajwa kuleta usawa katika ulipaji wa kodi na kuongeza ajira zaidi Lakini chama cha Republican kinasema sheria hiyo itawanufaisha watu wote. Makamu Rais Mike Pence alitoa matokeo ya kura hizo. Katika mswada huu, kura 51 zinas...

Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo

MTEULE THE BEST Image caption Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ameitaka Marekani kuacha kwa muda mazoezi yake ya kijeshi nchini humo mpaka kumalizika kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika mapema mwakani. Anasema hii itasaidia pia kuifanya Korea Kaskazini kutotilia shaka uwepo wa wanamichezo wake kwenye michuano hiyo. Korea Kusini itakua mwenyeji wa michezo hiyo itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang mwezi Februari ikiwa ni kilomita 80 kutoka mpaka wake na Korea Kaskazini. Mapema Canada na Marekani ziliapa kuendeleza mazoezi hayo ili kuisukuma Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nyuklia. Image caption Vikosi vya jeshi la Korea Kusini na Marekani vikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na mpaka wa Korea Kaskazini Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kufuatia mpango wa matumizi ya mabomu ya Nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini. Michuano ya Olimpiki ya majira ya bariki inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo...