Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake

John Bolton amepewa jukumu la kupanga jinsi ya kuniangamiza' Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akizungumza na wanahabari mjini Caracas Desmba 12,2018 Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amedai kuwa Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake. Amewaambia wanahabari kuwa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani John Bolton, anahusuka moja kwa moja na njama hiyo japo hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo. Rais Trump amemtaja Maduro kama kiongozi wa kiimla na kumwekea vikwazo. Mapema wiki hii maafisa wakuu wa Urusi na Marekani walijibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumatatu katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Madur...

Moto wateketeza ghala la tume ya Uchaguzi

Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza ghala la tume ya uchaguzi nchini Congo. Sehemu ya Ghala lililoteketea, kwa moto. Inasemekana kuwa Mashine zaidi ya 7000 za kura na vifaa vingine vilikuwemo kwenye ghala hilo la Kinshasa ikiwa ni masaa kadhaa tangu Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) ilipotangaza kupokea vifaa mbalimbali vya uchaguzi ikiwemo mashine za kupigia kura. Kampeni za kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinaendelea baada ya kuanza rasmi Novemba 22, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 23 mwezi Desemba. Tume hiyo ya Uchaguzi ilisema kuwa imeorodhesha wapiga kura milioni 40 wanaotarajia kushiriki uchaguzi huo katika vituo vya kupigia kura 80,000 ambavyo vitakuwa na 'mashine za kupigia kura" zaidi ya 100,000. Kampeni zinaendelea wakati huu, kukiwa na mvutano mkubwa kuhusu suala la matumizi ya mashine za kupigia kura, pamoja na changamoto za kiusalama, mashariki mwa nchi hiyo. Wanasiasa wa upinzani, akiwemo mmoja wa wagombea w...

Tanzania yatia saini ujenzi wa mradi wa umeme unaopigiwa kelele na wanamazingira, Rais Magufuli asema ni mradi wa lazima kwa maendeleo

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stigler's Gorge ni jambo la lazima. Leo rais wa nchi hiyo John Magufuli ameweka saini na wakandarasi wa mradi huo kutoka Misri wakiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi yao. Hatua hiyo inakuja baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka mto Rufiji ambao unaweza kuzalisha megawati 2,100 kufanyika wakati huo Tanzania ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere. Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa na fedha za watanzania wenyewe kwa kiwango cha dola za kimarekani bilioni 2.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi trilion 6.5 za kitanzania. Na kampuni itakayofanya kazi hiyo inatoka Misri. Rais Magufuli amesema kwamba walitumia muda kutafakari kuhusu mradi huu kwa sababu Tanzania imebarikiwa na vyanzo vingi sana vya uzalishaji umeme kama vile maji,gesi asilia,upepo,joto ardhi ,makaa ya mawe pamoja na madini ya urani. Na kufikia uamuzi huo wal...

UMILIKI WA NDEGE WAWANYIMA USINGIZI MASTAA WA BONGO

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva na moja ya kiongozi katika kundi la Tip Top Connection, Madee Alli 'Seneda' ameelezea tamaa yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi katika maisha yake. Msanii, Madee (kushoto) na Mwanasoka, Mbwana Samatta (kulia) Madee amesema kuwa ana ndoto ya kumiliki ndege katika maisha yake kiasi cha kumnyima usingizi wake kila siku. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Madee ameandika, " ndoto inayosumbua usingizi wangu ," huku akiwa katika picha inayomuonesha akitembea kuelekea kwenye ndege ndogo. Kauli hiyo ya Madee kuhusu kumiliki ndege inakuja miezi michache baada ya nyota wa soka nchini anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta kueleza matamanio yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi. Septemba 12, Samatta katika ukurasa wake wa Instagram aliandika, " ndoto za kumiliki 'Private Jet' zimeanza baada ya kupiga picha hii, sio kila ndoto inaweza kutimia ila acha vita ianze ". Kwakuwa wote ni watu m...

BANGI KUTUMIKA HADHARI SASA

Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? Sehemu mbalimbali duniani mtazamo kuhusiana na matumizi ya mmea wa cannabis yaani bangi unabadilika kwa kasi. Serikali mpya ya Mexico ina mpango wa kuhalalisha matumizi ya bangi kama njia ya kujiburudisha, sawa na ilivyofanya utawala mpya wa Luxembourg. Wakati huo huo, viongozi wakuu nchini New Zealand, wanakusudia kuandaa kura ya maoni ya namna watakavyoshughulikia swala hilo. Jinsi maoni ya umma - na yale ya serikali- yanavyobadilika, ni dhahiri kuwa mataifa mengi yatafuata mkondo huo. Maswali yanayoibuka ni kwa namna gani nchi hizo zitadhibiti matumizi na usambazaji wa mmea huo? Ni nini hasa kinachopelekea mataifa mbalimbali katika kulegeza kamba kwenye sheria zake, au hata kuamua kuidhinisha ,matumizi ya bangi moja kwa moja? Vita dhidi ya mihadarati Ilikuwa mwaka 2012 ambapo Uruguay, ilipoandika historia kwa kuwa taifa la kwanza duniani kuruhusu matumizi ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha. Hatua hiyo, ...

Kitambulisho cha Vladimir Putin akiwa jasusi wa KGB chapatikana Ujerumani

Vladimir Putin alikuwa na umri wa miaka 33 alipopewa kitambulisho hicho Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini Dresden. Rais huyo wa Urusi amekuwa mara kwa mara akisema anajivunia kazi aliyoifanya akiwa kama jasusi wa idara ya ujasusi ya Urusi wakati huo ikifahamika kama KGB jijini Dresden miaka ya 1980. KGB kwa kirefu ni Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Kamati/Idara ya Usalama wa Taifa) Putin, wakati huo, alipewa kitambulisho na idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Muungano wa Usovieti (USSR). Idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ilifahamika kama Stasi, lakini kwa kirefu ni Ministerium für Staatsicherheit kwa maana ya maajenti wa Wizara ya Usalama wa Taifa. Kitambulisho cha Stasi alichokitumia Putin kimegunduliwa wakati wa uchunguzi kuhusu ushirikiano wa karibu uliokuwepo kati ya KGB na Stasi. Putin ambaye wakati huo...

Tupolev -160: Ndege za kuangusha mabomu za Urusi zatua Venezuela na kuighadhabisha Marekani

Ndege aina ya Tupolev Tu-160 iliyotua uwanja wa Simón Bolívar Jumatatu Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumattau katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho ni sawa na "serikali mbili fisadi kufuja mali ya umma." Serikali ya Urusi imesema maneno yake hayo "hayafai hata kidogo." Ruka ujumbe wa Youtube wa Минобороны России Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo Mwisho wa ujumbe wa Youtube wa Минобороны России Ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja...