Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Tanzania :- Marekani na Uingereza zatilia shaka 'haki za Binadamu kisheria'

Tamko la Marekani na Uingereza linagusia kesi ya Erick Kabendera kama mfano wa hivi karibuni Ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania." Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria. "Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo. "Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria k...

MBWANA SAMATTA KUCHEZA EPL

Mbwana Samatta atajiunga na EPL? Klabu ya Brighton inayocheza ligi ya Primia ya England inaongoza msururu wa klabu zinazomuwania mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta. Klabu nyengine za England ambazo zinamuwania Samatta ni Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza Samatta ana thamani ya Pauni milioni 12. Samatta ambaye bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na mabingwa wa Ubelgiji KRC Genk pia amezivutia klabu za Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa. Mshambuliaji huyo ambaye aliongoza kwa kupachika mabao msimu uliopita nchini Ubelgiji ameweka wazi kuwa anataka kuelekea nchini England msimu ujao. "Kwa sasa hivi siwezi kusema sana, ni kitu ambacho kipo kwenye mchakato nasubiria kitakapokuwa tayari na wakati utakapofika nitaweza kukizungumza. Lakini sijioni tena Genk, namuomba Mwenyezi Mungu litimie, lakini ikishindikana bado nina mkataba na Genk," aliiambia runinga ya Azam TV ya Tanzania wiki iliyopita. Romelu Lukaku: ...

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi

Neymar ameifungia PSG mabao 23 katika mechi 28 msimu huu Real Madrid imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27. (Sky Sports) Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar, 27, inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal) Manchester United wako tayari kulipa £81m ambayo itawawezesha kumnyakua mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV - via Mail) Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail) Leroy Sane (Kulia) Beki wa Chelsea Mbrazil David Luiz, 32, ataruhusiwa kujiunga na Arsenal kwa £8m tu. (Mirror) Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akipingiwa upatu kuhamia...

Michael Job: Je ni kweli kwamba mhubiri anayefananishwa na Yesu Kristo amefariki?

Michael Job, mhubiri wa Marekani na muigizaji ambaye hivi majuzi alizuru Kenya na kuitwa 'Yesu bandia' hajafariki kama ilivyoangaziwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania na Kenya. Kulingana na uchunguzi wetu jamaa huyo yupo hai na mzima wa afya. Kadhalika, mhubiri huyo yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa na vyombo hivyo vya habari. Taarifa za vyombo hivyo ambazo zilianza kuenezwa  siku tano zilizopita zinadai, Yesu huyo bandia alifariki siku chache tu baada ya kuhudhuria ibada ya kidini. Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa Michael Inadaiwa kwamba alifariki siku chache tu baada ya kutembelea taifa hilo la Afrika mashariki baada ya kuuguwa ugonjwa wa mapafu. Hata hivyo mhubiri huyo ameendelea kupakia mtandaoni picha na video ya shughuli zake siku baada ya siku. Picha na video za karibuni zaidi alizipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook saa nne usiku wa kuamkia leo. Katika chapisho hilo na kanda za video alizoweka katika akaunti...

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

Mabadiliko ndani ya Simba SC Tanzania ni muamko mpya?

Mmiliki mwenza wa Simba SC Mohammed Dewji anijtahidi kuona klabu hiyo inakuwa ndani na nje ya uwanja (Picha kwa hisani ya Mahmoud Bin Zubeiry) Siku ya Jumanne mashabiki wa mojawapo wa timu kongwe Tanzania watakusanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kusherehekea "Simba Day". Ni katika kuidhinisha wiki ya Simba au kwa umaarufu "Simba Week" na inahusisha mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia pamoja na mechi za timu za wanawake walio chini ya miaka 20. Shughuli zilizopangwa kwa siku saba zimenuiwa kuongeza ukaribu na ushirikiano baina ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo pamoja na Simba kuisaidia jamii kupitia miradi tofuati. Ni sehemu ya azimio la Bilionea Mohammed Dewji, mmiliki mwenza wa klabu hiyo anayeitaka klabu hiyo ikuwe ndani na nje ya uwanja ili kuhakikisha ufanisi zaidi. "Niliwahi kukutana na mojawapo ya viongozi wa Zamalek (mnamo 2003) na niligundua wakati huo kuwa bajeti ya Zamalek ni mara 50 zaidi ya baj...

Mfumo wa nyota na sayari unaounda dunia umepinda

Picha mpya za falaki yetu ya Milky Way Mfumo wetu wa sayari na nyota, ama falaki, upo katika umbo la upinde na si nyoofu kama ilivyodhaniwa hapo awali, utafiti mpya umebaini. Njia hiyo ya falaki, maarufu kwa lugha ya Kiingereza kama Milky Way, katika vitabu vyote vya sayansi na taaluma inaoneshwa ipo katika unyoofu. Hata hivyo, utafifiti mpya wa nyota zing'aazo zaidi kwenye falaki hiyo umebaini kuwa nyota hizo hazipo kwenye njia nyoofu, zimepinda. Wataalamu wa unajimu kutoka Chuo Kikuu cha Warsaw wanadhani kuwa nyota hizo zimepinda kutoka kwenye njia nyoofu ikiwa ni matokeo ya kutangamana na falaki nyengine za karibu. Ramani mpya tatu za falaki ya Milky Way zimechapishwa kwennye jarida la Science . Picha maarufu zaidi ya Milky Way ikiwa katika mstari nyoofu imetokana na utafiti wa nyota milioni 2.5 kati ya nyota zipatazo bilioni 2.5 katika falaki hiyo. Dr University. "Undani wa kimfumo na historia ya falaki ya Milky Way bado kabisa kujulikana, na moja ya saba...