Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Kim Jong-un akabidhiwa mpango wa kushambulia Guam

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha AFP Image caption Wanajeshi wa Korea Kaskazini wanasubiri agizo la kushambulia kisiwa cha Guam Kiongozi wa Korea Kaskazini amepokezwa habari kuhusu mpango wa taifa hilo wa kutaka kurusha kombora hadi katika kisiwa cha eneo la pacific cha Guam kinachomilikiwa na Marekani kulingana na ripoti za vyombo vya habari. Lakini ripoti hiyo imesema kuwa itachunguza vitendo vya Marekani kabla ya kuchukua hatua ya kurusha kombora hilo katika kisiwa cha Guam. Wiki iliopita, Korea Kaskazini ilionya kwamba mikakati inawekwa kushambulia eneo ambalo ndege za kijeshi za Marekani zimekita kambi. Kumekuwa na cheche za maneno kati ya Marekani na Korea kaskazini. Rais wa Korea Kusini aiomba Marekani kuzuia vita Marais wa Marekani na Korea Kusini wazungumza Vita Vikuu vya Dunia vinakaribia? Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini Ripoti hiyo ya kitengo cha habari cha KCNA ilisema kuwa Kim Jong un aliutazama mpango huo kwa muda mrefu na kuujadili na ma...

Mrithi wa Mugabe apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha AFP Image caption Makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa Mmoja ya watu wanaotarajiwa kumrithi rais Mugabe wa Zimbabwe amekimbizwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu kulingana na chombo cha habari cha AFP. Emmerson Mnangangwa ambaye ni makamu wa rais wa Zimbambwe alikuwa mgonjwa ghafla wakati wa mkutano wa hadhara siku ya Jumapili. AFP imemnukuu waziri wa Afya David Parirenyatwa akisema: Anaendelea kupata nafuu. ''Alikuwa akitapika na kuharisha na kukosa maji mwilini. Amefanya vipimo vingi''. Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amesema kuwa atatetea wadhfa wake wakati wa uchaguzi wa mwaka ujao

Zuma: Kulikuwa na njama za kutaka kuniuwa

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha AFP Image caption Rais jacob Zuma wa Afrika kusini amesema kuwa kulikuwa na njama za kutaka kumuua Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini wikendi iliopita alizungumzia kuhusu jaribio la kumuua akisema kuwa aliwekewa sumu na karibu afariki kutokana na msimamo wake wa kiuchumi na marekebisho ya umiliki wa ardhi. Niliwekewa sumu na ningefariki kwa sababu Afrika Kusini ilijiunga na Muungano wa Brics unaounganisha mataifa ya Brazil, Urusi, India, China na jamii ya kibiashara ya Afrika kusini chini ya uongozi wake. ''Walisema nilikuwa nina mpango wa kuharibu nchi'', alisema Zuyma. Akihutubia mkutano wa wanachama wa ANC huko Phongolo, Kwa Zulu Natal siku ya Jumapili, rais huyo alisema kuwa alilengwa alipotaka kuweka kwa marekebisho makali ya kiuchumi. Kulingana na ripoti hiyo kulikuwa na majaribio matatu ya kumuuwa. Katika kanda hiyo hakusema ni nani aliyejaribu kumuua lakini anasema ni mtu wake wa karibu

Raila Odinga kufichua madai ya wizi wa kura Kenya

MTEULE THE BEST Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais uliopita ameliambia gazeti la Financial Times nchini Uingereza kwamba atafichua ushahidi siku ya Jumanne kuhusu vile alivyoibiwa kura. ''Tutauonyesha ulimwengu ulivyochezewa'' . Bwana Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne pia alibaini kwamba hatowania tena urais na kwamba aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo. ''Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, Sitawania urais tena......tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu haujui kinafanyika''. Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta. Madai hayo hatahivyo yamepuuziliwa mbali na tume ya uchaguzi

Makubwa ya Magazeti ya TZ leo August 15..Udaku, Michezo

MTEULE THE BEST Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 15 2017 kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.

Mvua zasababisha maafa Sierra Leone

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Madhara yaliyosababishwa na mvua nyingi Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu mia tatu. Inaofiwa kwamba miili zaidi iko chini ya vifusi. Jitihada za kuokoa zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia. Rais Ernest Bai Koroma amesema kupitia televisheni kwamba vituo vya dharura vimewekwa ili kukabiliana na kile alichokiita janga la taifa. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Maporomoko ya udongo Shirika la Msabala mwekundu limesema inakadiriwa zaidi ya watu laki tatu wamepoteza makazi yao. Eneo lililoathirika zaidi wilaya ya Regent iliyopo pembezoni mwa mji wa Freetown baada ya mlima uliojaa maji kuporomoka

Zaidi ya watu 250 wafariki dunia kwa maporomoko

MTEULE THE BEST Image caption Maporomoko ya ardhi yafukia watu wengi Sierra Leone Idadi ya watu waliouwa kwnye maporomoko ya ardhi nchini Sierra Leone haujulikani baada ya idaia tofauti kutolewa. Shirika la habari la AP linasema kuwa takriban watu 250 wameuawa. Eneo moja la milima liliporomoka mapema leo Jumatatu kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi kufukiwa kwa mjibu wa mwandishi wa habari wa BBC Umaru Fofana Makamu wa rais nchini Sierra Leone Victor Bockarie Foh, alisema kuwa kuna uwezekano kuwa mamia ya watu wameuawa akiongeza kwa idadi ya watu waliouawa huenda ikaongezeka. Maporomoko ya ardhi yauwa 15 China 100 hawajulikani waliko Maporomoko ya ardhi yaua watoto 44 Colombia Mwandishi wa habari aliye eneo hilo anasema kuwa watu wemgi walipatwa wakiwa bado wamelala wakati maporomoko yalitokea Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mafuriko yamekuwa makubwa "Mke wangu amekufa, watoto wangu wote wamekufa, Leo asubuhi niliongea na watoto...