Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Wavulana wavalia sketi shuleni Uingereza

MTEULE THE BEST Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wamefika shuleni wakiwa wamevalia sketi kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo. Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule yaLonghill eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20 wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi badala ya suruali ndefu. Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na wengine kutengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na kuvalia suruali ndefu hawakuadhibiwa. Lakini badala ya kuvalia sare kamili ya wakati wa masomo, kama walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa wamevalia sketi. Image copyright ANGELA PARKER Image caption Michael Parker, mmoja wa wanafunzi, akiwa na kaptura na akiwa na sketi Watatu waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni. Mwalimu mkuu Kate W...

Mkenya aliyekamatwa Tanzania afungwa miaka 20

MTEULE THE BEST Mahakama moja nchini Kenya imemfunga jela Feisal Mohammed, anayetuhumiwa kwa ulanguzi wa pembe za ndovu, kifungo cha miaka 20 gerezani. Pia Feisal ametozwa faini ya dola 200,000. Alipatikana na hatia ya kulangua vipande 413 za pembe za ndovu, vyenye thamani ya dola 400,000. Hakimu Diana Mochache, wa mahakama ya mji wa Mombasa, alisema kuwa ushahidi uliashiria kuwa Feisal ndiye mmiliki wa vipande vya pembe vya ndovu, vilivyopatikana kwenye bohari moja jijini Mombasa yapata miaka miwili iliyopita. Image caption Feisal Mohammed (kulia) akishauriana na mawakili Hakimu alitaja ulanguzi kama uhalifu mbaya, na kwamba walanguzi wa pembe sharti wafungwe ili kukomesha mauaji ya ndovu. Ameongeza kuonya kuwa ulanguzi usiposimamishwa, huenda vizazi vivayo vikapewa hadithi tu kuhusu jinsi ndovu walivyokuwa, sawa na jinsi vizazi vya sasa vinapewa hadithi za wanyama waliokuwa wakiitwa dinosaur. Wanne wengine waliokuwa wameshitakiwa pamoja naye Feisal waliachiliwa. ...

Mourinho adokeza Pogba atatua Man Utd

MTEULE THE BEST Jose Mourinho ametoa kidokezo cha karibuni zaidi kwamba Manchester United wanataka kumnunua tena Paul Pogba kutoka Juventus ya Italia. Mourinho amesema “mmeona moshi, jueni kuna moto”. United wanadaiwa kutoa £100m, ambayo ni rekodi ya dunia, kumnunua mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 23. Image caption Pogba alipokuwa Manchester United Pogba aliondoka Old Trafford mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 19. Manchester United walilipwa £800,000 pekee na klabu hiyo ya Italia. Image copyright GETTY "Sitawafanya kuwa watu wasiojua na kutaka kuwaonesha kwamba hatujaribu kumnunua mchezaji mmoja,” amesema Mourinho. Meneja huyo kufikia sasa amenunua wachezaji watatu: beki Eric Bailly kutoka Villarreal, kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund na mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic. Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumnunua Pogba, Mourinho alisema: “Tulijiwekea malengo matatu, tulipata watatu na tutampata huyo...

Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya

MTEULE THE BEST Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo. "Watu wengi wamekuwa wakiduwazwa na gari hili mitaani hapa jijini Nairobi, na wengi wamependezwa nalo," anasema Francis Romano, msimamizi wa kampuni Knights Energy, inayohamasisha watu watumie magari ya aina hiyo. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo hii ikiwa na maana kwamba hazitoi moshi au gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani kwa hivyo yanafaa mazingira. Ndege ya kisasa ya Ethiopia yatua Kenya Aidha, mwenye gari haathiriwi na kupanda na kushuka kwa bei ya mafuta. Linaendeshwa kwa njia karibu sawa na gari la kawaida. Hata hivyo gari hilo lina uwezo wa kusafiri umbali wa takriban kilomita 90 hadi 135 kabla ya betri zake kuisha chaji, kasi yake ya juu zaidi ikiwa kilomita 180 kwa saa. Upungufu mwingine ni ukosefu wa vituo vya kuchaji gari hilo, na huenda ukakwama ukiwa katika maeneo ya mashambani ambapo ha...

Watu sita wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye bunduki waliowafyatulia risasi watu katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani.

MTEULE THE BEST Watu sita wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye bunduki waliowafyatulia risasi watu katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani. Polisi wanasema washukiwa bado hawajakamatwa na wamewatahadharisha watu na kuwashauri kutotoka nje. Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea katika jumba la kibiashara la Olympia, ambalo linapatikana mtaa wa Moosach, kaskazini magharibi mwa Munich. Watu walioshuhudia tukio wanasema wamewaona watu watatu waliokuwa na bunduki. Maafisa wa polisi Bavaria wamekuwa katika hali ya tahadhari tangu Jumatatu kijana mhamiaji alipowadunga visu na kuwajeruhi watu kadha katika treni, shambulio ambalo kundi la Islamic State lilidai kuhusika. Polisi wamesema shambulio hilo ni la kigaidi. Wanasema habari za kwanza kuhusu ufyatuaji wa risasi kwenye jumba hilo linalopatikana katika barabara ya Hanauer zilitokea muda mfupi kabla ya saa thenashara jioni. Image copyright Kituo kikuu cha treni katika mji huo wa Bavaria kimefungwa...

wosia kwa kijana wako hakika hatapata mke bora

MTEULE THE BEST MWAMBIE KIJANA WAKO KUWA 1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema. 2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari. 3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao" 4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe! 5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza. 6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio! 7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali. 8. Mwanamke anaweza kukusa...

Mke bora anatimiza haya katika ubinti wake

MTEULE THE BEST TIMIZA HAYA UTAKUWA MKE BORA wosia wangu kwa madada zetu 👉  Mwili wako sio Maonesho, kila mwanaume auone. 👉  Mwili wako sio Mdoli kila mwanaume Auchezee. 👉  Mwili wako sio dampo, upokee kila uchafu wa mwanaume. 👉  Mwili wako sio Mali ya umma kila mwanaume akutumie. 👉  Mwili wako sio kiburudisho, kila mwanaume Ajiridhishe. 👉  Mwili wako sio pazia la Sebuleni, kila mwanaume Akufunue. 👉  Mwili wako sio karanga za kutembezwa mtaani kila mwanaume Akuonje Utamu wako. 🔹  Mwili wako ni wa Thamani sana. Mwili wako ndio utu wako. 🔹  Ebu Tunza Mwili wako nao Ukutunze. Uheshimu Mwili wako nao Utakuheshimisha. 🔹  Si kila mtu wa kuushika Mwili wako. Usitumie Mwili wako kama kitegauchumi, Usitumie Mwili wako kama dhamana ya kupata vile unavyohitaji. 🔹  Usitumie Mwili wako kama Njia ya kupata Mume Atakayekuoa. Kama Mungu amepanga Uolewe utaolewa tu dada yangu hata bila ya kufunua Sketi yako. Muamini Mungu Yeye nd...