MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Image caption Raia wengi wapo katika hali mbaya kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu Umoja wa Mataifa umetoa wito kusimamishwa kwa muda mapigano katika mji wa Ragga nchini Syria, kuruhusu idadi ya raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka. Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, anasema mji wa Raqqa yawezekana kwa sasa ni moja kati maeneo hatari duniani na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kutoa mwanya kwa raia kutoroka katika eneo hilo. Amesema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki kama kinga ya kivita. Hata hivyo idadi hiyo ya raia wapatao 25,000 kwa wamekwama ndani ya mji huo huku kukiwa na mfululizo wa mashambulizi ya anga kwa juma moja lililopita. Image caption Ragga unatajwa kuwa miongoni mwa miji hatari zaidi duniani Shirika la kimataifa la Amnesty linasema mamia ya watu wameuawa tangua mashambulizi hayo yalipoanza katika mji wa Raqqa mwezi june mwak...