FAHAMU KWANINI MWANAUME HUMWAGA SHAHAWA USIKU AKIWA AMELALA/USINGIZINI.
FAHAMU KWANINI MWANAUME HUMWAGA SHAHAWA USIKU AKIWA AMELALA/USINGIZINI. Mwanaume kumwaga mbegu akiwa usingizini huitwa ndoto nyevu (nocturnal emission) au kwa lugha ya kawaida kumwaga bila kukusudia usiku. Hili ni jambo la kawaida, hasa kwa wanaume vijana na hata watu wazima. Sababu kuu huwa ni za Kisaikolojia, Maumbile na hata Mihemko ya mwili. Nimekuwa naletewa kesi hii na Wanaume wakijua labda ni Matatizo yao ya Ki-Afya au laa Wanavamiwa na Majini mahaba. Ni kweli kuna nafasi ya kuvamiwa na Pepo wa ngono hao jini mahaba lakini pia kuna pepo wa Kingono wajulikanao kama Sexual Transmitted Demons huwavamia Wanaume kwa wanawake pia lakini njia hii huwa ni tofauti na kuota ndoto nyevu. Zifuatazo ni Sababu za kwanini Mwanaume Humwaga Mbegu za Kiume akiwa Usingizini ama laa akiwa amelala hata inapokuwa Mchana. 1. Kwanza ni matokeo ya Mwili Kujisafisha. Mwili wa Mwanaume hutengeneza mbegu (manii) kila siku, Kama hajafanya tendo la ndoa wala kufanya punyeto yaani kujichua kwa muda mrefu...