Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2020

SIMIYU YAJIPANGA KUPAMBANA NA COVID-19

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  mkoa umetenga shule za Sekondari za Bweni za Serikali kuwa maeneo ambayo yatatumika kuwahifadhi washukiwa wa Virusi vya Corona  endapo watapatikana mkoani hapa;  baada ya serikali  kufunga shule na vyuo nchini kwa siku 30 lengo likiwa kukabiliana na ugonjwa huo. Mhe. Mtaka ameyasema hayo wakati akipokea mchango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya  shule ya sekondari Anthony Mtaka uliotolewa na umoja wa madhehebu ya kikirsto Lamadi na kuongeza kuwa mbali na maeneo ya shule Mkoa pia umetenga maeneo ya hoteli ambayo yatatumika endapo washukiwa/watu wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huo ambao hawatahitaji kukaa kwenye maeneo ya shule. "mkoa hautatumia hoteli kwa ajili ya kuhifadhi mtu yeyote atakayeshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona badala yake tutatumia shule za zetu za sekondari za bweni lakini ikitokea mtu anahitaji kukaa hotelini tayari tumeandaa hoteli za kutosha"alisema Mtaka. " ...
       

CORONA| EPL, LIGUE 1, BUNDESLIGA, LALIGA, UEFA, UUROPA , ITALY, N.K ZASIMAMISHWA

Coronavirus : Mechi za Ligi ya soka ya England kuahirishwa hadi tarehe 3 Aprili Mechi za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi tarehe 3 Aprili kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona. Mashindano yote Ligi ya soka ya Ulaya, mkiwemo Championi Ligi na Ligi ya Ulaya, mechi ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus. Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa. Katika Championi Ligi, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa. Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa. Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa. Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatol...

PICHA| UZINDUZI WA KARAKANA YA KUU YA JESHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua karakana kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) - Lugalo jijini Dar es salaam. Machi 13, 2020

RAIS WA TANZANIA ATOA TAHADHARI KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORANA

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani. Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana ya jeshi hii leo jijini Dar Es Salaam. Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo. ''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.'' ''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua na hatua zimeanza kuchukuliwa waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''. ''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga...