MTEULE THE BEST Wanaume wa wanawake kutoka Kenya ndio warefu zaidi eneo la Afrika Mashariki kwa wastani kwa mujibu wa utafiti ambao matokeo yake yametolewa leo. Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la eLife yanaonesha kimo cha wastani miongoni mwa wanaume wa Kenya ni sentimeta 169.64 na wanaume sentimeta 158.16. Utafiti huo ndio wa kina zaidi kufanywa, kwa mujibu wa watafiti hao, na uliangazia matokeo kutoka utafiti 1,472 uliofanywa katika mataifa 200. Ulifuatilia kimo cha watu waliozaliwa mwaka 1896 hadi wale waliozaliwa mwaka 1996 ambao walitimiza umri wa miaka 18 mwaka 1914 hadi mwaka 2014. Waliochunguza kote duniani ni watu 18.6 milioni. Kimo cha watu hutegemea lishe anayopata mama akiwa mjamzito pamoja na lishe ya mtoto anapokuwa mchanga. Kimo cha mtu huhusishwa sana na afya ya mtu kwa jumla pamoja na hali ya maisha. Mataifa yenye watu warefu zaidi duniani yaorodheshwa Watu warefu kwa kawaida huishi maisha marefu na huwa hawana mat...