Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Kimbunga Hurricane Matthew chaua watu 100 Haiti

MTEULE THE BEST Image caption Miti iliyong'olewa na kimbunga hicho Siku mbili baada ya kuipiga nchi ya Haiti, kimbunga Hurricane Matthew kimeendelea kusababisha madhara makubwa hususan maeneo ya Kusini Magharibi mwa nchi hiyo. Idadi ya watu waliokufa imefikia 100 wengi wakiwa ni kutoka mji wa Roche-à-Bateau na Jeremie. Image caption Picha ya kbla na baada ya kimbunga hicho Nyumba nyingi zimeharibika vibaya, huku wakaazi wake wakiachwa bila chakula na maji. Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa asilimia 80 katika baadhi ya maeneo zimehariwa vibaya, miti imengooka na mazao yamezolewa na maji.

Mugabe kuondoa sheria kandamizi ya uwekezaji Zimbabwe

MTEULE THE BEST Image caption Rais Mugabe anataka kuona uchumi wa nchi hiyo ukiimarika Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amaeeleza mipango ya kuondoa sheria ambayo inalalamikiwa na wengi kwa kushindwa kutoa nafasi kwa wawekezaji wa nje. Sheria hiyo inayataka makampuni mbalimbali ya kimataifa kutoa hisa nyingi kwa raia wa Zimbabwe. Kwa sasa sheria hiyo haina nguvu sana na Rais Mugabe anataka kuona uchumi wa nchi hiyo ukiimarika. Sheria hiyo inalalamikiwa vikali na mashirika ya fedha ulimwenguni IMF kwa kusababisha kuanguka kwa uchumi wa Zimbabwe. Kumekuwa na maandamano dhidi ya serikali katika miezi ya hivi karibuni, kutokana na kudorora kwa uchumi wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

Colombia huenda ikakosa pesa za msaada kutoka Umoja wa Ulaya

MTEULE THE BEST Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa unaweza kusitisha kutoa fedha za maendeleo ambazo zilitengwa kwa ajili ya kuisaidia Colombia kufuatia kukwama kwa juhudi za kusitisha mapigano yaliyodumu kwa nusu karne. Pesa hizo ambazo ni kiasi cha karibu euro milion 600 zilitengwa kwa ajili ya kuisaidia serikali mjini Bogota kusitisha mapigano ambayo yamedumu kwa nusu karne, na kuangamiza maisha ya baadhi ya watu. Kwa zaidi ya saa nne Rais Santos kwa nyakati tofauti alikutana na maraisi wa zamani Andres Pastrana na Alvaro Uribe kujadili hoja ambazo zimesababisha kukataliwa kwa makubaliano hayo ya amani ambayo yamesainiwa na Rais Santos pamoja na waasi wa FARC Pastrana na Uribe wanataka kufanyika kwa mabadiliko katika makubaliano hayo wakisisitiza masharti magumu kwa waasi wa FARC, ambao makubaliano ya sasa yanawahakikishia nafasi 10 katika bunge na kupunguziwa vifungo kwa wapiganaji watakaokiri makosa yao. "Tunaweka wazi mabadiliko ya awali ambayo ni lazima yazingat...

Antonio Guterres kuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

MTEULE THE BEST Waziri mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa baada ya kupigiwa kura nyingi kuliko wagombea wengine katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Baada ya duru ya sita ya kura isiyo rasmi katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Antonio Guterres anatarajiwa kutangazwa rasmi Alhamisi kuwa Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa. Guterres ambaye alikuwa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR kwa miaka kumi iliyopita, alipata kura 13 kati ya 15 za nchi wanachama wa baraza hilo la usalama huku nchi zote tano wanchama wa kudumu walio na kura ya turufu wakimuunga mkono. Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin alitangaza kuwa ni bayana kuwa Guterres ndiye atachukua wadhifa unaoshilikiwa na Ban Ki Moon mwenye umri wa miaka 72, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Korea Kusini ambaye anakamilisha mihula yake miwili ya miaka kumi kati...

Kina dada wa Chelsea wapewa kichapo na Wolfsburg Stamford Bridge

MTEULE THE BEST Image copyright REX FEATURES Image caption Zsanett Jakabfi akifunga dhidi ya Chelsea Matumaini ya kina dada Chelsea kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya yamefifia baada yao kulazwa 3-0 na kina dada wa Wolfsburg uwanjani Stamford Bridge. Kiungo wa kati kutoka Hungary Zsanett Jakabfi alifunga mabao yote matatu mechi hiyo na kuiweka klabu hiyo kutoka Ujerumani kwenye nafasi nzuri ya kusonga kutoka hatua ya klabu 32. Chelsea, ambao kwa sasa wanaongoza ligi kuu ya kina dada Uingereza, walionekana kulemewa kipindi chote cha mechi hiyo iliyotazamwa na mashabiki 3,783. Wolfsburg, waliofika fainali msimu uliopita, watakuwa wenyeji mechi ya marudiano tarehe 12 Oktoba. Klabu hiyo imetwaa ubingwa mara mbili tangu msimu wa 2012-13. Chelsea walishindwa kwa jumla ya mabao 4-1 na Wolfsburg hatua ya klabu 16 bora msimu uliopita.

Hisia kali zatolewa kuhusu filamu mpya ya Bruce Lee

MTEULE THE BEST Image caption Muigizaji wa Hong Kong Philip Ng akimuigiza Bruce Lee katika filamu kuhusu historia yake. Mashabiki wa nyota wa filamu za Kichina Bruce Lee wamekosoa filamu mpya ya nyota huyo inayopotosha kuhusu maisha yake. Filamu hiyo 'Birth of the Dragon' inaonyesha maisha ya nyota huyo alipokuwa mdogo nchini Marekani pamoja na pigano lake lililozua utata dhidi ya bwana Wong Jack Man mwaka 1964. Filamu hiyo ilioelekezwa na George Nolfi ,ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika sherehe ya filamu ya Toronto. Lakini mashabiki wengi wamepinga vile inavyomuonyesha Bruce Lee,wakisema kuwa nyota huyo alishushwa sana hadhi yake katika filamu inayozungmzia maisha yake yeye mwenyewe. Image copyright BBC SPORT Image caption Filamu hiyo kwa jina Birth of The Dragon ''Huu ni utani? Nilikuwa hapa umuona Bruce Lee,lakini wakati mwingi wamekuwa wakimuonya mtu mmoja mweupe'',aliandika mtumiaji wa IMDb ticklegear katika shambulio la mtanda wa kijamii....

Mwalimu mkuu wa shule alikopigwa mwanafunzi Tz asimamishwa kazi

MTEULE THE BEST Image caption Walimu waliokuwa wakimshambulia mwanafunzi nchini Tanzania Serikali ya Tanzania imeagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kanda ya video ilioonyesha kundi moja la walimu likimpiga mwanafunzi. Mwalimu mkuu wa shule hiyo tayari amesimamishwa kazi kwa mda kwa kutochukua hatua hata baada ya kugundua kuhusu kisa hicho ,taarifa ya serikali imesema. Raia wa Tanzania katika mitandao ya kijamii walionyesha hasira zao ,wakiitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya washambuliaji hao. Video hiyo ambayo haijakaguliwa inaonyesha mwanafunzi mmoja akipigwa na kundi la walimu katika kile kinachoonekana kuwa chumba cha wafanyikazi wa shule. Katika kanda hiyo ya sekunde 38,takriban watu watano wanaonekana wakikabiliana na kushambulia mvulana huyo aliyeanguka chini kwa kumpiga ngumi pamoja na mateke. Adhabu ya kupigwa viboko ni haramu nchini Tanzania,na kisa hicho cha hivi karibuni kinatarajiwa kuzua mjadala kuhusu utekelezwaji wa sheria hiyo katika shule za taifa ...