Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

TRUMP : KOREAKASIKAZINI WANAHUSIKA NA KIFO CHA OTTO

MTEULE THE BEST Rais wa Marekani Donald Trump ameutaja utawala wa taifa la Korea Kaskazini kuwa wa kikatili kufuatia kifo cha mwanafunzi mmoja wa Marekani ambaye alikuwa amefungwa jela kwa zaidi ya miezi 15 nchini humo. Korea Kaskazini ilimrudisha nyumbani Marekani, Otto Warmbier mwenye umri wa miaka 22 wiki iliopita ikisema kuwa alikuwa hana fahamu kwa kipindi cha mwaka mmoja na kwamba ilikuwa ikimsaidia kibinaadamu. Wazazi wake wanasema kuwa aliteswa vibaya. Otto Warmbier aaga dunia Korea Kaskazini yamwachilia huru Mmarekani Mwanafunzi aliyeachiliwa na Korea Kaskazini alazwa hospitalini Korea: Tulimwachilia mwanafunzi kwa misingi ya kibinadamu Bwana Warmbier ambaye alifungwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwa hoteli moja hakuweza kupata fahamu tena. Haki miliki ya picha EPA Image caption Otto Warmbier alipokamatwa baada ya kujaribu kuiba bango la propaganda Bwana Trump alisema kuwa kifo cha Warmbier kimeimarisha mipango ya utawala wake wa kutaka...

shambulio la mtandao lilifanywa na korea kasikazin

MTEULE THE BEST Nani alihusika katika shambulio la kirusi cha mtandaoni ambacho kiliathiri kompyuta katika zaidi ya mataifa 150 duniani, zikiwemo Kenya na Tanzania? Kumeibuka madai kwamba huenda wadukuzi walitoka Korea Kaskazini. Lakini kufikia sasa, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha hilo. Huenda hujawahi kusikia kuhusu kundi linaloitwa Lazarus Group, lakini pengine unafahamu baadhi ya matokeo ya shughuli zake. Kundi hili lilihusika katika kudukua mfumo wa kompyuta wa Sony Pictures mwaka 2014 na tena wakadukua benki moja ya Bangladesh mwaka 2016. Inasadikika kwamba wadukuzi hao wa Lazarus Group walifanyia kazi yao China lakini kwa niaba ya Korea Kaskazini. Wataalamu wa usalama mtandaoni sasa wanahusisha shambulio la kirusi cha WannaCry na kundi hilo baada ya ugunduzi uliofanywa na mtaalamu wa usalama wa kompyuta wa Google Neel Mehta. Mehta aligundua kwamba maelezo ya kutunga programu ya kompyuta ya kirusi cha WannaCry yanafanana na maelezo ya programu zilizowahi...

MAJAJI WA MAHAKAMA KUU WA HACHA KAZI NA MKUU WA MKOA

MTEULE THE BEST Majaji wawili wa Mahakama Kuu nchini Tanzania wameacha kazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu. Taarifa hiyo inasema majaji Aloysius Kibuuka Mujulizi na Upendo Hillary Msuya wamewasilisha maombi ya kuacha kazi kwa rais, ambayo yamekubaliwa. Jaji Mujulizi alikuwa pia mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadiki pia ameacha kazi. Taarifa ya ikulu haijaeleza sababu iliyowafanya maafisa hao watatu kuamua kuomba kuacha kazi.

RAIS WA MAREKANI AFICHUA SIRI KUU ZA IS KWA URUSI

MTEULE THE BEST Haki miliki  RAIS wa Marekani Donald Trump alifichua taarifa zinazofaa kuwa siri kuu kuhusu kundi linalojiita Islamic State (IS) kwa waziri wa mambo ya nje wa urusi, vyombo vya habari nchini Marekani vinasema. Taarifa hizo, zilihusu kutumiwa kwa laptopu kwenye ndege, na zilitoka kwa mshirika wa Marekani ambaye hakuwa ametoa idhini kwa habari hizo kukabidhiwa Urusi, gazeti la Washington Post linasema. Bw Trump alikutana na Sergei Lavrov katika afisi yake wiki iliyopita. Mshauri mkuu wa usalama wa taifa wa Marekani HR McMaster amepuuzilia mbali madai hayo kwenye vyombo vya habari na kusema ni ya "uongo". Tuhuma kwamba huenda maafisa wa kampeni wa Bw Trump waliwasiliana na maafisa wa Urusi zimegubika utawala wa rais huyo, na kufikia sasa uchunguzi unaendelea Lakini rais amepuuzilia mbali tuhuma hizo na kusema ni "habari za uongo". Wakati wa kampeni, Bw Trump alimkosoa sana mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton, kwa jinsi...

JAY Z AMPA JINA ALLY KIBA HUKO LONDON

MTEULE THE BEST Mtandao mkubwa wa kuuza muziki wa TIDAL ambao upo chini ya rapa Jay Z umempa jina jipya msanii kutoka Bongo Alikiba na kumtambua kwa jina la 'The unstoppable' yaani mtu asiezuilika kwa kitu akifanyacho.  Msanii Alikiba wakati akifanya mazoezi kabla ya kufanya show nchini Uingereza wikiendi iliyopita. "The unstoppable AliKiba is live right now in London"  mtandao wa TIDAL uliandika wakati Alikiba akifanya yake kwa steji usiku huo.  Alikiba alipewa jina hilo wakati akishiriki katika moja ya tamasha la muziki ambalo lilifanyika mwisho wa wiki nchini Uingereza ambalo lilikusanya mastaa kibao akiwepo Cassper Nyovest, P Square, Davido, Awilo Logomba, Sarkodie, Tekno , MI na wasanii wengine wengi huku bongo ikiwakilishwa na 'King' Alikiba ambaye alipata nafasi ya kufanya 'performance' ya ngoma zake kama Mwana, Unconditionally Bae na Aje. Mashabiki wengi wameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo ...

Mkewe rais wa Nigeria Aisha Buhari amesema kuwa mumewe sio mgonjwa sana zaidi ya inavyodhaniwa

MTEULE THE BEST Mkewe rais wa Nigeria Aisha Buhari amesema kuwa mumewe sio mgonjwa sana zaidi ya inavyodhaniwa. Alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kuwa Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 74 anaendelea na majukumu yake na kwamba amekuwa akikutana na mawaziri. Kundi moja la watu mashuhuri lilimtaka rais Buhari kuchukua likizo ya matibabu kufuatia wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya. Mnamo mwezi Machi alirudi nchini Nigeria baada ya likizo ya matibabu iliochukuwa wiki saba nchini Uingereza ambapo alitibiwa ugonjwa usiojulikana Wakati aliporudi nyumbani alisema kuwa hajawahi kuwa mgonjwa sana maishani mwake. Rais huyo hajaonekana hadharani kwa kipindi cha wiki moja sasa, na hatua ya kutohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri pamoja na ibada ya kila wiki ya Waislamu inayofanyika siku ya Ijumaa, imesababisha uvumi zaidi kuhusu hali yake ya kiafya, kundi hilo la watu 13 limesema katika taarifa. Bi Buhari alishutumiwa na mumewe mwaka uliopita aliposema ka...

Duke suruali kuto oa

MTEULE THE BEST Spika wa bunge katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, amesema kwa umma utaombwa kutoa maoni yake kuhusu mswada wenye lengo la kuwazuia wanaume maskini kuoa zaidi ya mke mmoja. Alhassan Rurum aliiambia BBC kuwa viongozi na wasomi wataombwa ushauri kuhusu ni tata t haswa atatambuliwa kuwa maskini. Sheria ya kuzuia wanaume kuoa wake wengi kutangazwa Nigeria Waliokamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwa Pendekezo hilo lenye utata lilitolewa na Muhammad Sanusi II, ambaye ni Emir wa Kano, kuhakisha kuwa wanaume wana familia ambazo wanaweza kuzitunza.