MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Virusi vya Zika vinaweza kutibu saratani ya Ubongo Virusi hatari vinavyoweza kusababisha madhara kwa ubongo wa watoto vinaweza kusaidia kwenye matibabu mapya kwa saratani ya ubongo kwa mtu mzima, kwa mujibu wa wanasayansi nchini Marekani. Hadi sasa virusi vya Zika vinaonekana tu kuwa tisho la afya duniani. Zika yazimwa Brazil Ugonjwa wa Zika waripotiwa Angola Lakini utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa virusi hivi vinaweza kuvamia na kuua seli zinazosababisha saratani ya ubongo wa mtu mzima. Majiribio yaliyofanyiwa panya yalionyesha kuwa virusi vya Zika vilikula seli za saratani ya ubongo. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Virusi vya Zika vinaweza kutibu saratani ya Ubongo Binadamu bado hawajafanyiwa utafiti huo, lakini wataalamu wanaamini kuwa virusi hiyo vinaweza kuingizwa kwa ubongo wa binadamu wakati wa upasuaji ili kuangamiza seli za saratani ya ubongo. ...