Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Awad Ibn Auf kwanini amejiuzulu

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan. jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi. Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia. Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007. James Copnal...

Mzozo Sudan: Baraza la kijeshi lawakamata waliokuwa maafisa wa serikali

Raia Khartoum wameapa kuendelea na maandamano mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji. Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumuidhinisha watakayemchagua. Maandamano ya miezi kadhaa nchni Sudan yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita Waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia Raia wanaendelea kuandamana na wamekita kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu Khartoum. Je baraza la kijeshi limesema nini ? Katika mkutano na waandishi habari siku ya Jumapili, msemaji Meja Jenerali Shams Ad-din Shanto ameeleza kwamba baraza la kijeshi lipo "tayari kuidhinisha" serikali yoyote ya kiraia itakayoidhinishwa na vyama vya upinzani. "Hatutomteua waziri mkuu. Watamchagua," alisema akimaanisha upinzani...

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Awad Ibn Auf kwanini amejiuzulu

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan. jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi. Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia. Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007. James Copnal...

Je Fidel Castro alikuwa mtu wa aina gani?

Fidel Castro aliitawala Cuba kama taifa lenye mfumo wa chama kimoja kwa takriban nusu karne Tawala za kijamaa zilianguka kote duniani , lakini Castro aliendelea kupeperusha bendera nyekundu karibu na maadui wake wakubwa, Marekani. Kiongozi huyo mwenye utata alisifiwa na wafuasi wake kama kiongozi wa ujamaa, askari mwanasiasa ambaye aliirejesha Cuba mikononi mwa watu. Lakini alikabiliwa na shutuma kwa kuwazima wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa na sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba. Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa tarehe 13 Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya mkulima bwanyenye , Angel María Bautista Castro y Argiz, ammbaye alihamia Cuba kutoka Uhispania. Mama yake , Lina Ruz González alikuwa kijakazi aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae alikuwa mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya kuzaliwa kwa Fidel, akawa mkewe. US LIBRARY OF CONGRESSImage captionBatista (Kushoto) aliungwa mkono na Marekani Castro alisoma katika shule ya kikatol...

Ripoti ya CAG yawasilishwa Bungeni Tanzania, asisitiza neno dhaifu ni la kawaida

Prof Mussa Assad ametiwa hatiani na Bunge kwa tuhuma za kudharau chombo hicho. Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania Prof Mussa Assad amesisitiza kuwa ataendelea kutumia neno dhaifu. Akiongea na waandishi wa habari baada ya ripoti zake kuwasilishwa Bungeni, Prof Assad amesema neno hilo ni la kawaida kwenye fani ya uhasibu. "Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia," Prof Assad amesema. Hata hivyo Prof Assad hakuwepo Bungeni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mkutano wake na wanahabari umefanyika kwenye ofisi yake mjini Dodoma. "Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma," amesema Prof Assad. Azam TV@azamtvtz “Kwa mwaka 2017 tulitoa mapendekezo 350, yaliyotekelezwa kwa ukamilifu ni mapendekezo 8...

David Beckham azungumza kiswahili

Aliyekuwa mchezaji wa kandanda wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham hajulikana kuwa na ujuzi wa kujua lugha nyingi lakini anaongoza kampeni dhidi ya malaria ambapo anaonekana akizungumza lugha tisa. Anaonekana katika filamu fupi akizungumzia vita dhidi ya Malaria na kupitia kamera na teknolojia ya tarakilishi anazungumza kiswahili, Kinyarwanda, Kiarabu, na kiarabu miongoni mwa lugha nyengine. Mdomo wake na uso unalingana na matamshi yake lakini sauti zinazosikika zinatoka kwa manusura wa ugonjwa wa malaria. Waandalizi wanatumai kwamba watu wengine duniani wataingia na kuongeza sauti zao. Sauti zitakazopatikana zitatumika kuwashinikiza viongozi duniani huku wakiandaa kufanya maamuzi kuhusu hazina ya kukabiliana na Ukimwi, TB na Malaria.

Teknolojia mpya yatumika kumnasa chatu mkubwa mwenye mimba Florida, Marekani

NATIONAL PARK SERVICE Hifadhi moja ya taifa Florida, Marekani imemnasa chatu mkubwa mwenye urefu wa futi 17 (mita 5.2) kwa kutumia teknolojia mpya ya kuwanasa viumbe wavamizi. Nyoka jike huyo, ambaye ndiye mkubwa zaidi kuwahi kunaswa kwenye hifadhi ya Big Cypress alikuwa na uzito wa kilo 63.5 na alikuwa na 'mimba' ya mayai 73. Chatu ambao ni wavamizi kwenye eneo hilo wanatishia pakubwa maisha ya viumbe wa asili wa jimbo la Florida. Watafiti katika hifadhi hiyo waliwategeshea vifaa maalum madume ya chatu ili kuwatafuta majike yanayopandwa na kukaribia kutaga. "Timu ya watafiti ilimfuatilia dume moja lililofungwa kifaa hicho na kumnasa jike huyo karibu yake," imeeleza taarifa ya hifadhi hiyo kupitia mtandao wa Facebook. Pamoja na kuondosha nyoka wavamizi, hifadhi hiyo inatumia matokeo ya tafiti zake ili kustadi tabia za nyoka na kutengeneza njia mpya za kukabiliana nao. Chatu wanachukuliwa kama viumbe wavamizi jimboni Florida toka walipoonekana kwa mara ya k...